Kulikuwa na kaka mmoja aitwaye Denis,alikuwa na mdogo wake aitwaye Faraja,Denis na Faraja walifiwa na wazazi wao tangu wakiwa wadogo.Denis alikuwa hajasoma na Faraja alikuwa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya sokoine.Alikuwa na rafiki yake aitwaye Dickson.Denis alikuwa anamsomesha mdogo wake kwa urithi walioachiwa na wazazi wao.
Siku moja Denis alikuwa anasafiri kuelekea Mwanza.alipokuwa akimuaga dada yake alimtahadharisha ajiepushe na marafiki wabaya hasa wavulana wadanganyifu ila alikuwa na rafiki yake aitwaye Dickson hvyo moyoni alifurahi sana kwamba kaka yake anasafiri kwahyo atapata wakati mzuri wa kukutana na rafiki yake huyo wa kiume.siku moja Dickson akapanga kumtembelea Faraja,lakini Faraja aliogopa kukiuka agizo la kaka yake ila kwa kuwa alimpenda sana alimwambia aje jumapili mchana.
Jumapili ilipofika Dickson akaenda kwa kina Faraja na mambo yakaendelea hivi;
Dick;hodi hodi!
Faraja;karibu
Dick;asante sana faraja
Faraja;vipi za toka jana
Dick;Nzuri
Faraja;(anawaza jinsi ya kumweleza kaka yake)
Dick;vipi faraja mbona kimya? Au hukufurahi ujio wangu?
Faraja;hakuna tatizo.unajua Dick humu ndani naishi na kaka yangu na leo anarudi kutoka safari yake na alinieleza kuwa hataki mvulana aje hapa.sasa sijui itakuwaje?
Dick;sasa itakuwaje?au niondoke asinikute?
Faraja;ngoja nikuambie kaka yangu hajui kiingereza sasa akija tu tutaongea kiingereza ili asituelewe sawa?
Dick;sawa dear.
Baada ya muda mfupi...
Denis;hodi hodi!
Faraja;karibu,nani?
Denis;ni mimi Denis
faraja;ah! Kaka Denis shikamoo!
Denis:marahaba! Ehe! Huyo ni nani?na nilikuambiaje?
Faraja;ni mwanafunzi mwenzangu amekuja kuchukua vitabu.
Denis;mpe haraka aondoke unasubiri nini?
Dick;naomba kile cha do you remember our promise!
Faraja;hicho sina labda kile cha yes l remember!
Dick;halafu kile cha jana cha at what time!
Faraja;kile nimeacha darasani labda hiki cha at four o'clock'
Dick;basi naomba kile cha where will we meet'
Faraja;kile nakitumia chukua hiki 'at the famous restaurant near the big supermarket'
Denis:yaani mpaka sasa hamjamaliza tu? Na hvyo vitabu vyote mtasoma siku moja?
Faraja:ndio kaka maana mwalimu atatutolea mtihani pale.
Dick:ehe! Vipi kuhusu kile cha don't forget our promise'?
Faraja:kile sina sikuchukua labda utapenda hiki cha don't worry!
Dick:asante sana faraja.kaka mimi ninaenda.
Hapa tunaweza kuona bila kuwa na elimu ni rahisi sana kudanganywa na watu hvyo elimu ni ufunguo wa maisha.

Categories:

Leave a Reply