Wiki hii ndio Jay-z na Kanye West wanatarajia kuachia albamu yao ya pamoja inayoitwa "Watch the Throne".
Pamoja na soko la muziki bado likiwa linaonekana kuwa gumu,ila Rappers wengi wanaonekana kuendelea kutengeneza mamilioni ya dola za kimarekani kupitia biashara nyingine mbali mbali ikiwemo na muziki pia.

Lile jarida maarufu la marekani limetoa orodha ya wasanii 20 ambao wameonekana kutengeneza pesa nyingi kupitia muziki. Na kama kawaida kwa miaka 3 mfululizo Shawn Cutter a.k.a Jay-z ameendelea kushikilia namba moja.
ORODHA YENYEWE NDIO KAMA IFUATAVYO:

1. JAY -Z
Jamaa akiwa anamiliki lebo ya muziki ya Roc Nation,migahawa ya 40/40,kampuni ya mavazi ya Roca Wear,ameendelea kushikilia namba moja na safari hii akiwa anatajwa kutengeneza kiasi cha dola za marekani 37 milioni.
2. P. DIDDY
Yeye mwaka jana alianzisha kundi lake la muziki la "Diddy Dirty Money" na akaachia albamu yake na kundi lake hilo iliyoitwa ''Last Train To Paris". Anatajwa kutengeneza kiasi cha dola za marekani milioni 35. Na anamiliki biashara mbalimbali ikiwemo kampuni ya mavazi ya Sean John,na ana hisa kwenye kinywaji cha Ciroc Vodka.
3. KANYE WEST

Jamaa ametengeneza kiasi cha dola za marekani milioni 16. Na yupo mbioni kuachia albamu ya pamoja na Jay-z itakayoitwa ''Watch The Throne"
4. LIL WAYNE

Akiwa ametoka jela mnamo mwaka jana mwezi novemba,lakini kutokana kufanya maonesho mengi ya muziki na pia kupitia kampuni yake ya muziki ya Young Money Entertainment,amefanikiwa kutengeneza kiasi cha dola za marekani milioni 15.
5. BIRDMAN a.k.a BABY

Yeye kwa pamoja na kaka yake anayeitwa Ronald Wiliams a.k.a Slim wanamiliki kampuni ya muziki ya Cash Money Records. Yeye anatajwa kutengeneza kiasi cha dola za marekani milioni 15. Kiasi cha pesa ambacho ni sawasawa na kile cha Lil Wayne ambaye ni mwanae wa kumlea.
WENGINE KWENYE ORODHA,NI HAWA WAFUATAO:

6. Eminem: $ 14 milion
7. Snoop Dogg: $14 million
8. Dr. Dre: $14 million
9. Akon: $13 million
10. Ludacris: $12 million

11. Wiz Khalifa: $11 million
12. Drake: $11 million

13: Pharrell Williams: $10 million
14. Timbaland: $7 million
15. Swizz Beatz: $6.5 million
16. Nicki Minaj: $6.5 million
17. Rick Ross: $6 million
18. 50 Cent: $6 million

19. Pitbull: $6 million
20. T-Pain: $5 million
20. B.o.B: $5 million

Ukitazama orodha hiyo hapo utaona kuna mwanamke mmoja tu ambaye ni Nicki Minaj kati ya wote 20 waliopo. Pia utaona wasanii wapya ambao wamepata umaarufu hivi karibuni kama B.o.B na Wiz Khalifa wakiingia kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza. Pia kuna wengine ambao wanaonekana kuporomoka,akiwemo 50 Cent na T-Pain. Wakati Drake akionekana kupanda juu,na The Boss mwenyewe Rick Ross akiwa pale pale.

Categories:

Leave a Reply