Soko la bidhaa zako linategemeana na aana ya bidhaa zako na walengwa katika soko lako. Kama huuzi bidhaa zako kwa watu walio mbali unahitaji kueneza ujumbe wako MATANGAZO kwa njia ya mdomo usione aibu kuwatangazia watu unafanya biashara yako, unaweza kutebngeneza business card na nyuma ya card zako unaeleza unachokifanya mbele unaweka jina lako na contact adress.Unaweza kuweka bango. Njia nzuri ya kutangaza biashara yako ni kutoa huduma nzuri. Mwisho ushauri wangu ni kwamba biashara ni matangazo huwezi kukwepa gharama hizo. Business Plan ni jambo la kwanza na la msingi katika uanzishwaji wa biashara yako. Mambo ya msingi unayotakiwa kufanya katika business plan yako ni kama ifuatavyo:

* Aina ya biashara unayokusudia kuanza
* Wateja walengwa kwa biashara yako wanaoishi maeneo hayo, wanaopita maeneo hayo nk.
* Eneo la kufanyia biashara yako ukitilia maanani kuchunguza ushindani wa biashara uliopo katika eneo hilo.
* Fanya utafiti na wafanyabiashra wengine ambao wana uzoefu na biashara hiyo ili kupata mwelekeo wa biashara yako.
* Fanya utafiti wa source ya kupata bidhaa kutoka makampuni yanayouza na tafiti ni kampuni ipi yenye maslahi kwako.
* Andaa mfumo wa gharama za uendeshaji wa biashara ikiwa ni pamoja na Mtaji wako,

* Gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na gharama za uanzaji wa bishara, vitendea kazi, kulipia pango, tax, umeme, usafiri, simu, mishahara, nk. (Kumbuka wewe unalipwa mshahara pia na umeajiriwa na biashara yako).

* Andaa jedwali la mapato na matumizi ya kila siku, juma mwezi hadi mwaka mmoja.

* Kisha tathmini faida utakayopata baada ya gharama za uendeshaji na kumbuka biashara inasimama ambayo ina net profit, gross profit tu ni hasara.pia

Mtaji ulio nao usiuhesabu kama ndio kianzio cha biashara yako, maana kuna gharama za maandalizi ya mahali utakapoweka biashara yako, leseni za biashara pamoja na vitendea kazi vingine. Hivyo vyote uvifanyie mahesabu katika gharama za uanzishwaji wa biashara yako.
Hakikisha theluthi moja ya mtaji wako wa pesa umebaki kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako maana biashara hadi isimame na kuanza kujiendesha yenyewe huchukua wastani wa miezi 6 kama upo eneo lenye wateja wazuri

Categories:

Leave a Reply