Tangu zamani mpaka sasa maisha ya binadamu yamekuwa ni mfumo wa mapigano Fulani kila siku ili kuyafikia malengo au madhumunin Fulani. Siku,miezi na miaka inapita mambo yanabadilika,dunia inabadilika na hata binadamu pia. Jinsi ulivyokuwa dakika kumi zilizopita ni tofauti sana na jinsi ulivyo sasa kutokana na mabadiliko yanayotokea katika kila sekunde na dakika.
Hivyo basi kila muda ukisogea lazima kuwe na mabadiliko Fulani katika mwili na mengine mengi. Kwa maelezo hayo kila mmoja ajue kuwa tunaishi katika dunia inayobadilika kila muda na inatupasa wote kuendana na mabadiliko hayo. Maisha ya mwanadamu ni mfumo wa mapigano kila siku ili kuendana na mabadiliko au kwa kifupi maisha ya mwanadamu hayana likizo.Kutokana na hayo maisha ni kutembea kwenda mbele ukisimama unapigwa na muda unaendelea na maisha yanaendelea.
s
afari ya maisha duniani huishia pale mwanadamu anapofariki tu hivyo basi kama bado unaishi maisha bado yanaendelea. Binadamu tuliumbwa ili kuyakabili mabadiliko ya maisha kila siku huku tukiendelea na mwisho wa siku Yule binadamu anayesimama kijasiri kuyakabiri mapito,magumu na matatizo yake ndiye anayefanikiwa kuyafurahia mema ya nchi na dunia. Na katika hili hakuna huruma.
Hakuna binadamu ambaye aliyakuta maisha ni mteremko kuishi hata wale wanaoishi maisha ya kurithi wakumbuke kuwa wapo walio yalipia gharama ya kuyakabiri. Hakuna binadamu mwenye likizo ya matatizo au misukosuko ya maisha duniani kila mmoja anapitia mtihani wa maisha yake hata wale wenye maghorofa makubwa na utajiri usio na kipimo wanapitia mitihani yao na zaidi wameyapitia magumu tena wengine wamepitia magumu kuliko hata yale wengine wanayapitia na kulalamika.
Na kadri siku zinavyosogea ndio mengi yanakuja lakini hayaji kummaliza binadamu bali kumwonyesha utamu wa maisha baada ya kuyakabili au hata kumtengeneza. Na hakuna tatizo lolote lisilo na jawabu, inawezekana halijaonekana bado lakini jawabu lipo hata yale matatizo makubwa duniani yana majibu pia kwani huu ndio mfumo wa maisha.Hivyo basi pale ambapo mhusika atakapoukubali ukweli inawezekana kupata jawabu kwa yote anayoyapitia ndo mwanzo wa safari ya kutatua kikwazo cha maisha yake inapoanza.
Na hata kama akikataa ukweli wa kuwa inawezekana haitabadili maana pia na atavuna anachoamini pia.
Ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa tangu zamani mpaka sasa na hata baadaye dunia itaendelea kuongozwa na watu wanaoukubali ukweli kuwa INAWEZEKANA na ndo hao ambao hufanya hata yale ambayo wengi huamini kuwa haiwezekani. Amini usiamini ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa inawezekana na itawezekana tu kwa Yule tu anayeamini na kukubali kuwa inawezekana.

Na Geophrey A. Tenganamba, kutoka katika kitabu cha “Kichwa Chako ni dhahabu ya utajiri”.
Vitabu kwa sasa vinapatikana Taglo twins internet café, Ubungo Oil com
na vinasambazwa katika bookshops au ukihitaji utaletewa mahali ulipo kwa gharama nafuu; bei Tsh.6000, mawasiliano; 0714477218, Email:gtlivemore@gmail.com


Categories:

Leave a Reply