Ndugu yangu mdau wa blog hii napenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa tena nafasi ya kuandika tena siku hii ya leo kama kawaida yetu na kwa maombi ya wengi kuwa na sehemu japo kwa wiki kuleta mahojiano au stori au historia ya mtu yeyote aliye fanikiwa katika maisha,
Leo nitaleta historia japo kwa kifupi juu ya ndugu yetu aliye tangulia mbele ya haki ,
ni mgunduzi wa kampuni ya Apple soma zaidi utamtambua huyu ninani na alikuwa na mchango upi katika dunia hii ya leo,
“Your time is limited, so don’t waste it living someone else’s life. Don’t be trapped by dogma – which is living with the results of other people’s thinking. Don’t let the noise of other’s opinions drown out your own inner voice. And most important, have the courage to follow your heart and intuition. They somehow already know what you truly want to become. Everything else is secondary.” SJ
Yawezekana ulipofungua ama kuingia kwenye mtandao kufanya lolote lile uliilotaka kufanya leo hii ukakutana na taarifa za kifo cha Steve Jobs, na kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta za Apple ama brauza ya safari utakuwa ulikutana na picha ya Bwana huyu ikieleza umri kuzaliwa na kufa kwake.

Bila shaka kama ulikuwa humjui au hukumfahamu hapo kabla leo utakuwa umemfahamu japo kidogo kupitia kifo chake, sina nia ya kukujuza juu ya msiba huu au umetokeaje na vitu kama hivyo, hapana, nia yangu ni kutaka tujifunze kwa pamoja sisi kama wajasiriamali juu ya mjasiliamali huyu asiyekata tama kirahisi. Jeni funzo gani tunapata kupitia historia ya maisha yake?
Tunachokiona ni kuwa toka akiwa mdogo alivutiwa na kutamani kujua zaidi juu ya mambo ya vufaa vya umeme, hapa ndipo alipojenga ukaribu na jamaa Mmoja aliyekuwa akifanya kazi kiwanda cha kompyuta HP Wakati huo, Woz akajenga mazoea kwenda kujifunza nyumbani kwa Woz, akajiunga naye na hatimaye akamua kununua sehemu ya mradi wa Woz wa Apple, akiwa na nia ya kutengeneza kompyuta bora kabisa duniani akiwa na umri wa miaka 20 tu.“Sometimes when you innovate, you make mistakes. It is best to admit them quickly, and get on with improving your other innovations.” SJ

Steve alianza kutengeza Apple nyumbani kwake na kuzitembeza madukani, waliweza kuuza japo kwa taabu kidogo kwani yao ilikuwa bodhaa mpya na soko limeshikiliwa na IBM, waliamua kuziongezea ubora kwa kuweka program zaidi na hatimaye baada ya muda walifanikiwa kukamata soko na hivyo miaka mine tangu kuanzishwa ikawa ni kampuni kubwa kiasi cha kuingia soko la hisa, mwaka wa tano walitengeneza faida kubwa kufikia Dola million 200, hivyo kuwa Millionea akiwa na miaka 25 tu.


Haya yalikuwa mafanikio makubwa sana kwa Steve, lakini pia yalikuja yakiwa yameambatana na majaribu yake, kwani kampuni ilianza kufanya vibaya kiasi cha kufikia kufukuzwa katika kampuni aliyoianzisha na kuamua kuuza hisa zake zote na kuendelea na maisha yake, lakini hakuuza maono wala ndoto zake.
“I’m convinced that about half of what separates the successful entrepreneurs from the non-successful ones is pure perseverance.” SJ
Huko msemo usemao “It is always dark before dawn” au ukiona kiza kimezidi kumekaribia kucha, pengine ndio unaoweza elezea mazingira ya kuibuka tena upya kwa Steve na hatimaye kufikia mafanikio aliyoyoacha nyuma yake.

Mwishoni mwa mwaka 1993 akiwa bado ana maono yake na ndoto zake zikiwa hazijaathiriwa na mawimbi ya mkwamo wa kibiashara alianza upya kuboresha bidhaa zake na hivyo kujaribu kuziuza upya kwa makampuni na vyuo, aliamua pia kutengeneza programu ya mwanasesere, alijaribu kutaka kuiingiza katika soko la hisa, akawaona wataalamu wa masoko na wachambuzi, walimcheka sana, walimwona kama anayeota ndoto ya mchana, kampuni yake ilikuwa ikifanya vibaya kwa kipindi cha miaka tisa mfululizo.
“I didn’t see it then, but it turned out that getting fired from Apple was the best thing that could have ever happened to me. The heaviness of being successful was replaced by the lightness of being a beginner again, less sure about everything. It freed me to enter one of the most creative periods of my life.” SJ
Hakukata tamaa, alikuwa na maono ya mbali na zaidi aliamini kuwa INAWEZEKANA, kutokana na kutokata tama kwake kwa jambo analoamini kuwa linawezekana, miaka miwili baadaye 1995 alipata mafanikio makubwa kupitia programu yake iliyokataliwa kwanza na wataaalumu na hivyo kumuingizia Dola Billioni 1.5, ikiwa ni mara tano zaidi ya alizowai kuingiza akiwa na Apple, huo ulikuwa mwanzo wa mafanikio na hatimaye kurudi tena Apple Macntoshi na kuendeleza ndoto yake ya kubadili ulimwengu kupitia teknologia.
“You know, I’ve got a plan that could rescue Apple. I can’t say any more than that it’s the perfect product and the perfect strategy for Apple. But nobody there will listen to me.” SJKutokana historia yake nimejifunza mambo mengi sana, hapa chini ni machache tu:-

  • Kufanikiwa katika jambo lolote maishani hakuna uhusiano na historia yako au hali ya uchumi ya wazazi wako.
  • Kufanikiwa kwako hakuna uhusiano wa moja kwa moja na elimu yako,
  • Kufanikiwa hakuna uhusiano na kazi unayofanya bali fikira na ndoto ulizonazo.
  • Kufukuzwa kazi si mwisho bali ni mwanzo wa kunoa akili na kutumia ubunifu wako kufikia ndoto zako.
  • Kushindwa (Failure) ni mwalimu mzuri sana maishani.
  • Kutokutaka tamaa, kung'ang'ania kile unachokiamini pasipo kujali wengine wanasema nini juu yake ndio msingi mkuu wa kutimiza ndoto zako. NK.
  • source:winners boulevard

Categories:

Leave a Reply