Ndugu zangu ni jumatatu nyingi tunakutana tena leo kwahiyo hatuna budi kumshukuru MUNGU kwa neema hii ya ajabu leo napendelea tuongeee kuhusu suala la kujiamini.
Jiamini wewe mwenyewe na kamwe usifikirie hatua ya kujihukumu na kujiona haufai miongon mwa jamii.kwasababu tu umeshindwa ktk jambo fulani,amini kwamba kama umeshndwa ktk jambo lolote,amini kwamba kama umeshndwa leo basi kesho ni yako ya mafanikio,usijilinganishe sana na waliokuzidi kimaisha licha ya kwamba wao ndio wakupe hasira zaidi ya kupambana,kumbuka kwamba kushndwa leo umeteleza tu haujaanguka,kwani waswahli wanasema kuteleza sio kuanguka na kwamba tunajifunza kutokana na makosa.kwa maana hyo ukiona umeshindwa kufikia malengo yako tambua kuwa umejifunza na sio umekwama.ktk kushindwa zaidi kupata ujuzi na kujisafisha ukizngatia haya kesho yako ya furaha inakuja mbele yako. BARIKIWA.

Categories:

Leave a Reply