Ndugu zangu napenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa tena nguvu na maarifa mimi na wewe kwa kukutana tena hapa siku hii ya weekend tulivu
Ndugu yangu leo kma kawaida kila siku za mwisho wa juma kama ilivyo maombi yenu kuwa tuwe tunaweka mahojiano au historia ya mu yeyote aliyefanikiwa,basi leo ninayofuraha leo kuwapo japo list japo kwa ufupi yawatu wanaoongoza kwa utajiri barani kwetu Afrika.
1.ALIKO DANGOTE
Mfanyabiashara kutoka Nigeria ambaye utajiri wake unatajwa kufikia kiasi cha dola za marekani bilioni 13.8.
Ni mmiliki wa Kampuni ya Dangote group na kwa kiasi kikubwa utajiri wake unatajwa kutokana na vyanzo mbalimbali kama vile kilimo,mafuta,gesi,saruji na ujenzi wa majengo.Ni tajiri wa kwanza Nigeria na tajiri wa 51 duniani.Kitu cha ajabu ni kuwa kwa mwaka jana tu utajiri wake uliongezeka kwa kiwango cha asilimia 557.
Anaishi Lagos Nigeria na Biashara zake anaziendesha Nigeria,Benin,Ghana,Cameroon South Africa na Zambia.
2.NICKY OPPENHEIMER
Jamaa kutoka South Africa ambaye utajiri wake unatajwa kufikia kiasi cha dola za marekani bilioni 7. Anatajwa kama tajiri wa kwanza nchini Afrika kusini na tajiri wa 136 duniani. Na utajiri wake unatokana na na madini akiwa anamiliki kampuni ya De Beers Diamond na ni mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Anglo American Plc ambayo inajihusisha na uchimbaji dhahabu.
3.NASSEF SAWIRIS


Anatokea nchini Misri na anatajwa kama tajiri namba moja huko Misri na kwa dunia ni tajiri wa 182. Na utajiri wake unafikia kiasi cha dola za marekani bilioni 5.6
4.JOHANN RUPERT


Ni tajiri wa pili nchini Afrika kusini na tajiri wa 219 duniani. Utajiri wake unafikia kiasi cha dola zqa marekani 4.8 ukiwa unatokana na umiliki wa kampuni mbalimbali Afrika Kusini na nje ya Afrika kusini.
5.NAGUIB SAWIRIS

Ni mdogo wa Naseef Sawiris,na anatajwa kama tajiri wa pili Misri na tajiri wa 310 duniani. Utajiri wake kwa kiasi kikubwa unatokana na kumiliki kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya Telecom ambayo imesambaa Afrika,ulaya,Mashariki ya kati na Asia.
Ndugu yangu ni hayo niliyo fanikiwa kukufumbua macho au kukukumbusha au kukutamanisha ili uweze kufikia mafanikio ya kweli
asanani sana na habari hii kwa hisani ya blog ya POPOTE TANZANIA.


Categories:

Leave a Reply