Katika Ulimwengu wa kipato na kujitafutia riziki watu wote tumegawanyika katika makundi makuu manne, Waajiriwa au Waliojiajiri, Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji, makundi hayo pia yamegawanyika katika pande kuu mbili, Kushoto na Kulia.

Upande wa kushoto kuna makundi ya Waajiriwa na Waliojiajiri, upande wa kulia ni Wamiliki wa biashara na Wawekezaji, mgawanyiko huu unatokana na wapi chanzo kikuu cha mtu mapato yake kinakopakina.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wasomi na wataalamu wa uchumi duniani, upande wa kushoto (Waajiriwa na waliojiajiri) ndio wenye watu wengi zaidi duniani asilimiam 95%, ndio wenye kipato kidogo zaidi, unalipa kodi nyingi zaidi, ulio masikini, wasio na uhuru na muda, kipato ama kukaa na familia zao, huku asilimia mkubwa wakiwafanyia kazi walio upande wa kulia na kumiliki asilimia 20 ya utajiri wa dunia.

Lakini upande wa Kulia, Wamiliki wa mifumo ya Biashara na Wawekezaji, ndio upande wenye watu wachache zaidi duniani asilimia 5% tu huku wakimiliki asilimia 80% ya utajiri woote wa dunia, huu ndio upande ambao kipato chao hakitegemei ufanyaji kazi wao moja kwa moja, wanalipa kodi chache, wana uhuru wa kipato, muda na pia kwenda popote watakapo na kufanya kazi na watu wawatakao.

Upande huu wa kulia unamiliki mifumo ya biashara na pia unatumia pesa kuingiza pesa kwa walio katika kundi la wawekezaji, hawa hawaitaji kuamka kila siku asubui kwenda kutafuta riziki, mifumo waliotengeneza uwawezesha kuwa na uhakika wa kipato hata kama yuko mbugani au ng’ambo na familia wakitalii kwa muda wowote ule.

Hivyo ukitaka kuwa na uhuru wa kipato, muda, mahali na kujikwamua toka kwenye umasikini pia unabudi kuanza kufikilia njia kukupeleka upande wa kulia, kuwa Mmiliki wa mfumo wa biashara ama Mwekezaji.

Wakati wa Zama za Viwanda (Industrial Age) karne iliyopita ilikuwa ni ngumu sana kufikilia kuwa mtu wa upande wa kulia angeweza kufanya juhudi au kupata njia kuhamia upande wa Kulia, ilikuwa ni ndoto, kama haukuzaliwa katika familia yenye utajiri basi ulikuwa na uhakika wa kubaki pale ulipo, upande wa Kushoto.

Habari njema ni kuwa ni rahisi sana kwa sasa, katika karne hii na Zama za Taarifa/Habari (Information Age) kwa mtu aliye upande wa kushoto kuweza kuhamia upande wa Kulia na kuwa Mmiliki wa mfumo wa Biashara na hatimaye kuwa Mwekezaji, kukua kwa teknolijia ya habari na mawasiliano, kumefanya ama kurahisisha mambo mengi sana, ikiwemo ufanyaji wa biashara, hivi sasa ulimwengu unashuhudia mamilioni ya matajiri wapya kila mwaka, Pual Zane Pilzer, Next Millionaireas, japo si rahisi sana kama vile mtu awezavyo kupata ajira ya kima cha chini.
Aina tatu za Madaraja.
Haya nadhani yanafaa kuitwa madaraja, ili mtu aweze kuhama kutoka upande wa kushoto na kuhamia upande wa kulia anaweza kutumia moja ya madaraja haya matatu, lengo kuu likiwa ni kujenga na kumiliki mfumo wa biashara, madaraja hayo ni:-

1. Traditional C-type Corporations- Huu ni mfumo wa kawaida wa biashara ama viwanda vya asili ambapo unajenga au kuanzisha biashara yako, mfano Bakhresa, Mengi, Mo Dewji, Mfuruki nk.

2. Franchises – Hii ni kununua mfumo uliopo tayari na kuendesha, mfano, Coca cola, Steers, Mc Donald, nk

3. Network Marketing – hapa unanunua mfumo uliopo na kuwa sehemu ya mfumo uliopo tayari.

Katika mifumo yote mitatu ama madaraja matatu yana nguvu na changamoto zake, changamoto kubwa kabisa katika daraja la 1 na 2 ni mtaji, mtaji mkubwa unaohitajika ili kuanzisha kampuni au kununua biashara itakoyoweza kuajiri watu wasiopungua 500 ili kuweza kuwa katika kundi la Wamiliki wa Mfumo wa Biashara.

Nguvu pekee iliyopo katika mfumo au daraja la tatu, Network Marketing ni mtaji mdogo unaohitajika kununua na kuwa sehemu ya mtandao mkubwa, makampuni mengi ya biashara ya mtandao utoa bure mafunzo ya biashara, vitendea kazi na nyenzo mbalimbali kumwezesha mtu kufanikiwa katika mfumo huu, huku ukipata fursa ya kuwa na biashara ya kimataifa, na hivyo kuwa Mmiliki wa mfumo huku ukijiandaa kuwa Mwekezaji.

“Network Marketing is really the greatest source of grass root capitalism, because it teaches people how to take a small bit of capital, that is your time and build the American dream” Jim Rhon

Daraja hili la Biashara ya Mtandao ndilo linapendekezwa na wanazuoni na wachumi wakubwa duniani, kwani kwa mtaji kidogo wa chini ya dola 1,000 mtu anakuwa mmiliki wa mtandao mkuubwa sana duniani, ukimpa mtu uwezo wa kufanya biashara popote duniani na yeyote pia, ni kama kuwa na duka lililowazi saa 24, siku saba za juma, inamfanya mwanamtandao kufanya kazi kwa bidii na smart na si kutumia nguvu kubwa mno kwa ujira kiduchu.
source:winners Boulevard

Categories:

Leave a Reply