BINADAMU tumezaliwa kuwaza kila wakati Mwanasaikolojia Alfred Binett mtaalamu wa mambo ya Intelligent Quotients (IQ) alisema kuwa ndani ya dakika moja binadamu huwa anawaza mambo mengi sana.

Kwa hiyo ili kufikia malengo na mikakati ya maisha yako unatakiwa kujitambua uko katika sehemu ipi hasa unapowaza mikakati ya maisha yako.

Usikubali kuyapa nafasi kubwa mawazo yasiyokuwa na manufaa katika maisha yako jitahidi kuyatupilia mbali na kukubaliana na mawazo ambayo yatakuletea manufaa, amini kuwa hujazaliwa masikini bali umezaliwa kuishi kutokana na unavyotaka.

Kumbuka kuwa mikakati ya mawazo yako ndiyo yatakufanya ufikie malengo, anza sasa kuwaza mafanikio hakika utaona.
SOURCE www. penzilakweli.blogspot.com

Categories:

Leave a Reply