Katika masuala ya kimaendeleo, kiasi kinachopatikana sehemu yake inatumika kwa matumizi ya kawaida (expenditures) na kiasi kikubwa kinatunzwa(savings) baada ya kutunzwa kiekezwe kadri ya mda au kiasi (investments).

1.Kuekeza kuko namna mbili; ya kwanza kwenye vitu vinavyoongezeka samani (asset) mfano nyumba, mashamba ya uzalishaji, mifugo, hisa, majengo ya kukodisha, n.k. (ukiona huna elimu ya biashara hii ni njia muafaka na risk yake ni ndogo.

2. Pili kwenye biashara yaani pesa inayozaa pesa yenyewe. Hii ni njia muafaka kwa wenye uzoefu wa kibiashara kwa sababu kama huna ujuzi kidogo kuna uwezekano ukarudi kwenye umasikini.

Matumizi ya vitu kama tv, simu ya bei, vitanda, sofa, n.k haya si utajiri haya ni matumizi ya kawaida tu.(expenditures). yanapaswa yafanywe pale tu umeshawekeza kwenye namba 1 juu au mbili au 1 na 2 kwa pamoja na kwa kiwango kadri ya uchumi unavyokua.

Ukiona huweki akiba, akiba unayoweka huiwekezi ila inakaa tu benki au nyumbani na baadae unaitumia inakwisha. hufanyi kabiashara hata kadogo na unafanya biashara usioweza kuidhibiti....basi hapo uajitazame upya ufanye marekebisho kwani bado kitafsiri uko ndani ya kitu kinaachoitwa na wataalam wa uchumi "mzunguko wa umasikini' au (VIRCIOUS POVERTY CYCLE).

Kujiondoa ndani ya mzunguko huo si jambo la mara moja lakini usome mtiriko hapo juu na fata taratibu hizo kidogo kidogo inawezekana.....

Categories:

Leave a Reply