Watu wengi udhani ama utafuta visingizio kwa kushindwa kwa kuendelea kimaisha, kutajirika au kufakiniwa na kudhani kuwa ni sababu mtu au watu fulani wanahodhi fursa zoooote za wao kutajirika na kuwa na mafanikio makubwa maishani, hiyo si kweli, ni dhana potofu na zaidi inaashiria uvivu wa kufukiri wa watu hao.


Katika dunia hii sooote tuna fursa sawa ya kupata vyote tutamanivyo ikiwa ni pamoja na utajiri, hakuna mtu anayeachwa kuwa masikini kwa sababu ya upungu au uchache wa utajiri, LAKINI MTU ANAACHWA KATIKA UMASIKINI KWA SABABU YA FIKRA ZAKE MWENYEWE.


Kuna fikra nyingi sana hasi na mapokeo zinazokumbatiwa katika jamii zetu ambazo ni kikwazo kikubwa cha mtu kusonga mbele au kuamua kuwa NATAKA KUTAJIRIKA, watu wanajifariji sana nazo, wanadhani ndio maisha Mungu amewapangia na kwamba hawana jinsi.


UKIAMUA kutofanikiwa utapata vijisababu viiiiingi sana, lakini ukiamua kuwa NATAKA kufanikiwa vijisababu vyoote hivyo vitakuwa kama ngazi kuelekea utakako.
source Bongo pix

Categories:

Leave a Reply