Woga ni adui mkubwa sana wa kufikia ndoto/MAONO yetu, Ni kibinadamu kuwa waoga, ni maumbile, lakini Ili mtu aweze kufanikiwa na kufikia ndoto zake unabudi kuushinda woga.
Nimejisikia leo kuzungumzia juu ya mada hii kutokana na uzoefu nay ale niliokutana nayo katika juhudi za kufikia mafanikio ama ndoto/maono.
Dr Napaleon Hill anasema:
“Every person comes into this world cursed, to some extent, with six Basic Fears, all of which must be mastered before one may develop sufficient self-Confidence to attain outstanding success.”
Dr Hill amechukulia woga kama ni laana ya aina fulani inayozuia mtu kufikia ndoto ama malengo yake, hiki ni kiwazo kikubwa sana, anasema sote tumezaliwa na aina sita za woga ambazo hatuna budi kuzishinda iwapo twataka kufikia malengo ama ndoto zetu maishani, haijalishi ni ndoto gani ulionayo ni muhimu kwanza uushinde woga.
Dr Hill anasema:
These Basic six Fears are:
1. The fear of Criticism
2. The fear of ill health,
3. The fear of poverty
4. The fear of old age
5. The fear of the loss of love of someone (ordinarily called jealousy)
6. The fear of death
The Fear of Criticism (Uoga wa kulaumiwa/kuchekwa/kudharauliwa/kukosolewa) ndio namba moja, wengi wetu tunaogopa kuelezea ndoto, maono au malengo yetu kwa kuogopa kuchekwa au kudharauliwa iwapo tutashindwa zetu.
Huu ni uoga mbaya sana hatuna budi kuushinda ikiwa tunataka kuona maono/ndoto zetu zinakuwa kweli.
Pindi utakapoweza kuushinda woga huu itakuwa ni rahisi kwako kuushinda woga mwingine na hivyo kuwa katika njia sahihi kuelekea mafanikio, maono ama ndoto zako.
“Most great people have attained their greatest success just one step beyond their greatest failure.” Dr Hill
Kila mmoja katika nafsi yake anayo labda picha au ndoto ya wapi au vipi anataka kuwa siku za usoni, pengine wengine wamekubali woga kufuta ndoto zao na hivyo kutakuwa na maono tena, hii ni hatari, kwani pasipo maono/ndoto ya nani au nini wataka kuwa maishani ni sawa na chombo kung’oa nanga bandarini pasipo kujua wapi kinapaswa kuelekea, matokea yake upepo utakipeleka popote na kitapotea bila shaka.
“Man, alone, has the power to transform his thoughts into physical reality; man, alone, can dream and make his dreams come true.” Dr Hill
Ndoto yangu ni kufikia Uhuru wa Kipato (Financial Freedom) ili niweze kuwa na uhuru wa kufanya kazi pale nitakapo na niwatakao, lakini pia niweze kwenda popote nitakapo duniani kwa wakati niutakao nikiwa na muda mrefu wa kuwa na familia yangu huku pato likizidi kila uchao, ni ndoto ambayo nataka iwe kweli, nashukuru Mungu kwa kunionesha njia ya kufikia ndoto hii.
“Success consists of going from failure to failure without loss of enthusiasm.”Winston Churchhill
source.nextbilionaire
Categories: