Kitabu changu nakiuza ofline na online tangazo lake ni kama ifuatavyo.

Kitabu cha Mbinu za biashara kinauzwa
Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
Mtunzi wa Kitabu hiki Charles P. M. Nazi ni Mkaguzi wa Hesabu Mwandamizi shirika la Umeme TANESCO mwenye uzoefu wa miaka 25 akiwa ni mtumishi wa umma.Ni msomi mwenye stashahada ya Uhasibu. Pia ni mshauri wa masuala ya biashara.
Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti na uzoefu katika kazi za ukaguzi alizozifanya kwa kuangalia matatizo ya uendeshaji wa biashara mbalimbali pamoja na ushauri alioutoa kwa watu walioomba ushauri kutoka kwake.
Kwa taarifa zaidi piga simu 255755394701

Charles ni mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara
Kwa ushauri tembelea blogu yangu http://www.squidoo.com/mshauricharles

Categories:

Leave a Reply