Ndugu mdau napenda kumshukuru MUNGU kwa mambo mema mengi aliyotutendea kwa muda wa mwaka huu wa2010 hatuna budi kumrudishia MUNGU SIFA NA UTUKUFU
ndugu mdau tunapokaribia kukamilisha mwaka huu yapo mambo mengi ambayo tulikuwa tumepangilia katika maisha yetu,yapo yaliofanikiwa na ambayo hayakufanikiwa na mengine yalikweb=nda kama tulivyokuwa tumepanga,
pamoja na hayo ndugu mdau hatupaswi kukata tamaa kwani tunapaswa kuamini kuwa hilo nalo litapita,pia matatizo yaliyotukumba mwaka huu yasitufanye turudi nyuma na tuone kuwa tumeshindwa hapana tunapaswa kusonga mbele kwani tuchukulie tatizo kama ni njia ya kutupeleka kwenye mafanikio yetu sisi.
ndugu mdau nakuakikishia kuwa tangu mwanzo kwenye mada zangu nimekuwa nikilisisitizia jambo hili kuwa MUNGU ametuumba ili tuje kufanikiwa na wala si kushindwa,hatupaswi kuwqa na mawazo ya kushindwa kwani kuwa na mawazo kama hayo nikuwa na mawazo ya kishetani,kwani siku zote shetani ana mawazo mabaya kwetu sisi wanadamu.
kwahiyo ndugu mdau wangu hatupaswi kukata tamaa pale tunapoona kuwa tumeanguka.
Ndugu mdau wangu kwa mwaka 2011 nimejiwekea malengo ya aina sita siyo vibaya nikashirikiana na wewe ndugu yangu angalau na wewe ukapata angalau njia y ni kwanamana gani unaweza kuweka malengo yako kwa mwaka 2011,na siyo lazima yafanane na malengo yangu ila najaribu kuonyesha japo njia hii inaweza kuwawezesha japo watu ambao hawawezi kujiwekea malengo kwahiyo ndugu nakupa japo kwa muktasari tu .
1=MALENGO YA KIMWILI>PHYSICAL GOALS
2=MALENGO YA KIFEDHA-FINACIAL GOALS
3=MALENGO YA KIROHO-SPIRITUAL GOALS
4-MALENGO YA KIKAZI-CAREER GOALS
5=MALENGO YA KIAKILI-MENTAL GOAL
6=MALENGO YA KIJAMII-SOCIAL GOALS
Ndugu mdau haya ni aina ya malengo yagu niliyojiwekea kwa mwaka2011,sikuweza kunyambua kwa undani ila kwa kadiri siku zinavyokwenda ntajitahidi kunyambua kimoja kimoja.
Ndugu mdau naona niishie hapa na nawatakieni mwisho mwema wa mwaka 2010
MUNGU AWABARIKINI WOTE

Categories:

Leave a Reply