Asante MUNGU kwa kunipatena fursa hii ya kuweza kuandika tena haya ambayo unaenda kuniongoza kuyaandika hapa naomba ee Mungu ukamuwezeshe msomaji wangu aweza kuelewa ambacho nimekiandika hapa
Ndugu yangu mdau leo nimeamua kukumbusha ili suala la huduma kwa wateja kwani nimeona baadhi ya wafanya biashara na watoa huduma wamelisahau nalo ni huduma kwa mteja
Siku zote napenda kusisitiuza kuwa mtoa huduma anapaswa kutambua kuwa mteja ni mtu muhimu sana katika biashara yake au huduma yake. Ndio maana unaona mpaka waswahili wana msemo wao unao sema kuwa MTEJA NI MFALME AU MALIKIA.
vilevile mtoa huduma anapaswa kutambua kuwa mteja ndiye anayemlipa mshahara pia anapaswa kutambua kuwamteja ni mtu wa kuheshimika sana,pia anapaswa kuelewa au kuzingatia yafuatayo
1>KUMJALI SANA MTEJA
2>KUMWONYESHA MTEJA TABASAMU
3>KUWA MVUMILIVU
4>KUWA MSAFI WAKATI WOWOTE
5>KUWA MBUNIFU WA HALI YA JUU SANA
Pia anapaswa kufanya haya mteja anapokuwa kwenye huduma yake,anapaswa kuelewa kuwa mteja anahitaji nini anapokuwa kwenye huduma yake
1>KUHESHIMIWA
2>KUPEWA KIPAUMBELE
3>KUPATA HUDUMA BORA
4>KUPATA MAELEKEZO MAZURI
Na nyongeza Mteja siku zote anahitaji maneno ya kushawishi na siyo ya kulazimishwa
pia siku zote mteja anahitaji kupata huduma inayokidhi mahitaji yake,kupat hguduma ambazo anatarajia na asizotarajia
Pia mtoa huduma hunapaswa kujua aina za wateja ni kamaifuatavyo
1>KUNA WATEJA WABISHI
2>KUNA WATEJA WEPESI KUNUNUA NA WAZITO KUNUNUA
3>KUNA WATEJA WABAHILI
4>WANAORIDHIKA NA WASIORIDHIKA HARAKA
kwa kuzingatia hayo yote niliyoyaandika japo sikutaka kufafanua kwa undani zaidi,ndugu yangu kwakuzingatia hayo kuna faida ambazo utazipata kwenye huduma yako nazo nikama ifuatavyo]
1>KUPATA ONGEZEKO LAKO KATIKA BIASHARA
2>KUONGEZA BEI NA WATEJA WASILALAMIKE
3>NI RAHISI KUPATA WATEJA WENGI
4>MWENYEBIASHARA AU HUDUMA UTAZIDI KUPENDWA NA KUFAHAMIKA ZAIDI
NA mwisho kama ni kijana kama mimi unaweza kupata mchumba
BARIKIWA.

Categories:

Leave a Reply