Kabla ya kusoma hii soma kwanza sehemu ya kwanza na ya pili.
Ahimidiwe Mungu Muumba kwa mambo mema mengi anayoendelea kunitendea.
Ndugu mdau leo ningependa kuendelea na mada yetu.ambayo inasema unajua kusudi la Mungu kukuleta hapa duniani?
Kitu nilichogundua katika mafanikio ni vita kubwa sana,kuna vita kubwa sana,kuna vita ya kurudishwa nyuma kwasababu mafanikio mara nyingi adui huwa anafurahi sana,kwahyo kuna njia nyingi sana za kukurudisha wewe nyuma ikiwemo za kukufanya wewe kuwa na fikra duni.anakufanya wewe ulale usingizi ambao hauna maana yeyote kwako,kwani kila unapotaka kukaa kufikiria kitu cha maana unapitiwa na usingizi,unapitiwa na wimbi kuwa litakalo kukupoteza wewe kumbukumbu,kwahyo wengi bado tupo kwenye mfumo wa maisha ya kubahatisha.
Kwahyo ndugu mdau,katika maisha ukitaka kufanikhwa lazima uwe na malengo madhubuti,pia hayo malengo madhubuti yanapangwa yanapangiliwa toka ktk hatua moja kwenda hatua nyingine usipofanya hivyo unaweza kuishi hv hv tu,ukawa unalala na kuamka tu kama mfanyakazi unawahi kazini unarudi kwahyo unajikuta una kaa bila kufikiria.
Tangu umeajiriwa umeshawahi kukaa na kujiuliza tangu uajiriwe umeshawahi kushika shilingi ngapi? Na katika hzo hela ulizowahi kupata umeshawahi kupata jambo gani la maana umeshawahi kufanyia?
Ndugu mdau kwaleo naishia hapa tukutane kwenye uwanja huu huu.
Barikiwa.
Categories:
Mungu azidi kukuinua katika kile ameweka ndani yako, kiachie wazi! kiwe NURU na msaada kwa wengine. Mungu akutunze
Amina dada Mary...
Na endelea kufuatilia mfululuzo huu wa masomo.