Nakushukuru Mungu muumba mbingu na dunia,kwa mambo mengi unayoendelea kunitendea mimi na ndugu yangu mdau.eeh Mungu narudisha sifa na utukufu.
Ndugu mdau leo nitataka nieleze kwa kifupi kuhusu hili la kukopesha wewe ukiwa kama mjasiri amali.
Ndugu mdau kukopesha kunaweza kuwa na faida au hasara,kwani kwa utafiti wangu nilioufanya kwa wajasiri amali kukopesha kunaleta madhara makubwa sana,kwani unakuwa unapoteza wateja,unapomkopesha mtu ni sawa na umemwambia asije tena kwenye biashara yako,unamwambia apunguze trip za kuja kwenye biashara yako,kwani huwa anabadilisha hata njia.kwahyo ndugu wajasiri amali uwe mwangalifu kuhusu ili suala la kukopesha,angalia usikopeshe kwa hasara,kwani kukopesha angalia mtu unayemkopesha kwani kukopesha inaweza kuwa fimbo ya kukuchapa wewe mwenyewe kwa sababu unampa mtu ambaye atakurudishia.
Categories:
samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.
http://blogutanzania.blogspot.com/
www.ringojr.wordpress.com
lakini ukikopesha basi mpe muda kadhaa na pia iwe na riba. Ila pia ni kweli lazima ujue unapokopesha ni nani unamkopesha
Kwanza habari za siku nyingi dada yasinta.
Unajua kumkopesha m2 unaweza kumpa masharti lkn pamoja na hayo bado tu kusumbulia lzma tu,na hata kama ukilipwa itakuwa si kwa Muda muafaka.
Sawa mkubwa ntafanya hvyo.karibu tena.
Kuna mchumi mmoja wa Afrika Magharibi anasema, kitu cha kwanza kukwepa maishani ni madeni. Anasema hakuna kisichofanyika bila kukopa.
Kinachopelekea mtu kukopa ni tamaa tu ya kupata vitu kabla ya wakati wake.
Na wakopeshaji kwa kulielewa hilo, wanatumia tamaa hizo kuwanyonya watu.
Kwa hiyo ingawa kwa upande moja inaonekana kama faida, lakini mkopo /deni laweza kuwa kitanzi cha hiari.
Kwel bwaya nakubaliana na hlo la huyo mwanauchumi.