Siku zote anayetoa huduma kwa mteja anapaswa kutambua kuwa mteja ni mfalme au malikia.
Vile vile atambue kuwa siku zote mteja hakosei,na vilevile atambue kuwa mteja ni wakuheshimiwa kila wakati,kwasababu mteja ndiye anayelipa mshahara anapaswa azingatie yafuatayo.
i-kumjali sana mteja.
ii-kumwonyesha mteja tabasamu.
iii-kuwa mvumilivu.
iv-kuwa msafi wakat wote.
V-kuwa mbunifu wa hali ya juu,vilevile anapaswa kufanya haya mteja anapokuwa kwenye biashara yako,anapaswa kutambua mteja anahitaji nini anapokuwa kwenye biashara yako.
i-kuheshimiwa
ii-kupewa kipaumbele
iii-kupata huduma bora.
Iv-kupata maelekezo mazuri
v-mteja anahtaji zaidi maneno ya ushawizi na sio ya kulazimisha.
Nb:mteja hanaitaji kupata huduma inayokidhi mahtaji yake,kupata huduma ambazo anatarajia na hasisotarajia kuzipata toka ktk biashara yako.
Vilevile mtoa huduma unapaswa kuelewa kuwa wateja wote hawako sawa wako wa aina mbali mbali,kwahyo siyo vibaya ukiangalia aina hizi za wateja.
i-wapo wateja wabishi.
ii-wepesi kununua na wazito kununua
iii-wabahili
iv-wanaoridhika na wasioridhika haraka.
Kwahyo ndugu yangu ukifanya hayo yote na ukiyatambua yote hayo utaona mabadiliko kwenye biashara yako.na utapata faida sana.hebu check faida za kumridhisha mteja.
i-kupata ongezeko lako ktk biashara.
ii-kuongeza bei na wateja wasilalamike.
iii-ni rahisi kupata wateja wapya.
iv-mwenyebiashara anazidi kupendwa zaidi na kufahamika zaidi.
v-utaweza kupata mchumba.
Barikiwa.
Categories: