Huimidiwe Mungu uketie mahali palipo inuka,nasema asante baba kwa kunipa fursa hii tena yakuandika tena nasema asante baba.
Ndugu wanablog karibuni tena ktk jamvi hli,naomba mada hii uisome kwa makini na kwa uelewa na utagundua kitu hapo
Mawasiliano kwa watanzania ni jambo la muhmu sana kwa watanzania wasasa kwani unaposoma vitabu vya dini vinasema kwamba,WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.na mimi naamini yapo maarifa ya aina tatu
-kuwa na maarifa ya kiungu.
-kuwa na maarifa ya ulimwengu wa chini.
-kuwa na maarifa ya ulimwengu huu wa kamaida, sasa maarifa haya ya ulimwengu wa kawaida ni maarifa ambayo wapendwa wengi wameyakosa,na wanashangaa kwanini maisha yao yanazidi kuwa magumu.kwani maisha yao hayajapata upenyo haya yote wanashindwa kutambua kuwa wanakosa maarifa ya kiulimwengu,maarifa tu ya kawaida,maarifa mazuri,ufahamu wa kifedha,maarifa ya mausiano,maarifa ya uongozi na maarifa ya kawaida ambayo kila binadamu anapaswa kuwa nayo,sasa wenzetu kule magharibi sasahv wanafanya juhudi sana ya kujiongezea maarifa haya binafsi.kwa ajili za maendeleo yao binafsi.wanaongezea kwenye elimu yao ya kawaida.lakini huku kwetu africa bado watu wengi tu hawajajua kwamba siri kubwa ya maendeleo ipo kwenye juhudi binafsi ,yapo kwako wewe mwenyewe kujisukuma kujiendeleza zaidi kusoma vitabu,kubroser kwenye internet kupata maarifa mapya.kukutana na watu wapya,kukutana na mawazo mapya,na vitu kama hivyo,hayo ni baadhi ya mambo unayotakiwa kuwa nayo yote kwa makini utaweza kuwabadilisha wengi sana, na hasa wewe binafsi.,haya ndio machache ambayo nimeweza kuyaandika kwako.unatakiwa wewe ubadilike kwanza ndio na mambo mengine yatabadika ,unajua kuna wengine wanataka labda company yake ibadilike kumbe hajagundua kuwa anapaswa abadilike yeye kwanza.lakini la msingi hapa ni kwamba ukibadilika wewe na mazingira yako yatabadilika,kipato chako akaunti yako ya bank.kwasababu wewe umedhamiria kubadilika.
BARIKIWENI.muwe na wikiendi nzuri.

Categories:

Leave a Reply