Napenda kumshukuru Mungu Muumba mbingu na nchi.kwa mambo mengi mema anayoendelea kututendea mimi na ww rafiki yangu mkubwa.
Nimambo mengi sana mwenyez mungu katujalia ktk mwaka huu 2008.mimi leo ningependa nitoe japo mchanganuo ambao utaweza kukuwezesha wewe ndugu mdau uwe na malengo ya mwaka 2009.nina mambo kama matatu hv ambayo naamini kabisa ukiyazngatia na kuyatilia maanani lazima utatoboza mwaka 2009.mambo yenyewe ni haya
1-Chukua karatasi andika mambo mazuri ambayo yamewahi kukutokea ktk maisha yako.
Ninaposema mambo mazuri namaanisha kama
afya njema
akili yako nk.
2-andika mambo ambayo mazuri ambayo watu wanakuzungumzia wewe,namaanisha mambo kama ,uzuri ulio nao,kuimba vzuri,bidii ktk kufanya kaz nk.
3-cha tatu na cha mwisho andika yale yote unayo yatamani,kama kununua nyumba,kujiendeleza kimasomo.nk
ukishayaandika haya yote utagundua nini malengo yako ya mwaka ujao.kumbuka mawazo yanaumba,na wewe ndiye nabii wa maisha yako mwenyewe
barikiweni
Categories:
malengo ni muhimu sana na yanaweka msingi wa maisha yako. kaka nimekutembelea leo naamini tupo pamoja kama samaki wa nyasa na mimi.
karibu nyasa tena sana
Asante bro kwakunitembelea kwenye blog yangu.naomba 2endelee kushirikiana bro.
Je mzima wewe, ahsante kwa kutukumbusha kuhusu malengo.
Kazi yako ni nzuri na nimeipenda.
Heri ya mwaka mpya, natarajia mwakani blog hii itakuja na mabadiliko makubwa ya kijamii.
kazi ni nzuri na imetulia, ujumbe umefika kiutambuzi.
Leo katika pitapita zangu nimejikuta nikiwa katika hiki kibaraza.
Blog imetulia na ina mafunzo mazuri.
Karibu kwangu tubadilishane uzoefu.
heri ya mwaka mpya
Salam,
Hii ni zaidi ya shule. Asante kwa kutupa somo murua litakalokuwa mwelekeo wetu kwa mwaka unaoanza saa chache zijazo. Mipango muhimu.
Nakutakia kila lililojema kwa mwaka unaoanza.