Kwanza namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kurudi tena hewani ngoja niende moja kwa moja kwenye mada yangu.
Kufanikiwa kwetu kuko mikononi mwetu sisi wenyewe,tusikae tukitegemea miujiza ya mafanikio,siku zote mafanikio hayaji hivi hivi bila juhudi binafsi,kwani kujituma kwetu ndio njia ya mafanikio yetu,kutokata tamaa kwani kukata tamaa ni mojawapo za njia ya kutukwamisha katika safari yetu ya mafanikio,halafu kuna hki kitu ambacho kinaitwa woga,woga ni adui mkubwa wa mafanikio,ukishaanza kuwa na woga kufanikiwa kwako ni sawa na ndoto kwa hiyo ndugu mdau tupigane tujipange sawa sawa ili tuweze kutunza malengo yetu,hakika tutatobozaaaa....
Barikiwa
Categories:
Ni kweli kabisa hakuna mtu au mungu siku moja atakuja na kukuambia e bwana we kazi ndio hii au ee bwa we nyumba ndio hii hapa ingia uishi. Ni lazima kujitegemea na kuna wengine wanategemea sana vya wazazi, ndugu yaani hawajagundua kuwa ni lazima kujitegemea kutumia akili yako, mikono yako na busara zako sio kutaka kirahisi tu. kazi kweli kweli
Kweli sister yasinta,unajua wengine wanapenda kubweteka na vyakupewa.
Pia wapo wale ambao ni waoga kufanya jambo lolote, pia wanaamini aliyesababisha kuwa na maisha duni labda ni baba yake, kaka zake na huendelea kulaumu kwamba nisingezaliwa familia maskini ningekuwa mbali sana au ningekuwa na wazazi ambao wangenisomesha basi ningekuwa mbali sana utadhani wote waliosoma wamefanikiwa.
Binafasi naamini kila mtu duniani anaweza kuwa vyovyote anataka kwa kadri anavyojiamini na kujituma mwenyewe na zaidi mtazamo wake na jinsi anavyowaza kwani adui mkubwa wa mafanikio ni kichwa chako.
Asante sana
Asante kwa mchango wako brother mbilinyi,karibu tena na tuendelee kutembeleana.