Napenda kumshukuru Mungu kwakunipa fursa tena ya kuiona siku hii ya leo.Kuna mambo mengi sana ambayo yanamkwamisha mtu yeyote katka mafanikio,kuna ambayo anayasababisha yeye mwenyewe au mtu mwingine, lakini hapa nitapenda kuzungumza na mtanzania yeyote yule mwenye uchu wa mafanikio kama mimi hapa,kuna mambo ambayo yanatu kwamisha,kwahyo sina budi kuyataja ili tupeane mbinu za kuweza kupambana na hivi vkwazo kwa mtazamo wa rafiki yangu aliyeniadithia mambo ambayo yanatu kwamisha sisi ni Kutokuwa na Maono makubwa,kutokuwa na maono makubwa inamaanisha kufikiria vidogo badala ya mambo makubwa,unajua nchi kama Nigeria ina watu wengi sana,ss kuna rafiki wa aliyenipa hii stori,anasema rafiki wake wanaigeria yupo chuo anasema cku moja alimuuliza unataka kuwa nani nayeye kwa ujasiri kabisa akamwambia anataka kuwa Raisi,just imagine nchi kama Nigeria yenye watu takribani milion mia na kitu anasema anataka kuwa Raisi? Kwa haraka haraka kwa hapa kwetu ninani mwenye maono ya namna hyo,hakuna kwanza asilimia kubwa ya Watanzania hatujijui sisi wenyewe ni kinanani,? Tunafuata mkumbo tu,nafikiri umeona maono makubwa yalivyo? Nisikuchoshe sana mdau,tutaendelea baadae hebu leta maoni yako.
Barikiwa

Categories:

Leave a Reply