Napenda kumshukuru Mungu Muumba mbingu na nchi kwa mambo makuu anayoendelea kutupigania.tunasema asante.Ngoja tuendelee na mada yetu hii. Biashara nyingi leo zinadumaa na kukimbiwa na wateja kwa sababu hii ya kutosikiliza malalamiko ya wateja wao.
Sijui kwanini wafanyabiashara hawajafikia mahali wakaweka sanduku la maoni ktk biashara zao.
Niliwahi kuona kauli mbiu fulani kwenye biashara moja.iliandikwa kwa lugha ya kingereza "if our service is good,tell others;but if is not good please tell us",(kama huduma zetu ni nzuri waambie wengine,lakini kama si nzuri samahani tuambie sisi)
mfanyabiashara ni mtumwa na mteja ni mfalme.nenda pande zote nne za dunia utakuta msemo huu.labda mfanyabiashara bandia.
Ni vigumu kusikiliza na kutendea kazi malalamiko ya wateja ktk hatua za awali
unachotakiwa kufanya ni kiasi cha kujifunza polepole hatimaye utafaulu na si ajabu ukajikuta unajilaumu mwenyewe badala ya kuwanyoshea wengine vdole ambao unadhani wanaiwangia biashara yako.
Hata kama kwa asili wewe si mpole au msikivu,jizoeze kufanya hvyo na siku ya siku utajikuta tabia hyo inafuata mkondo.
Jambo lolote ni kujifunza kama ulivyojifunza kutumia simu ya mkononi,basi hvyo hvyo jifunze kuisoma saikolojia ya mteja wako nawe utatoka kibiashara.

Categories:

Leave a Reply