Ahimidiwe Mungu mkuu,MUNGu Aketie maali palipo inuka,Mungu mpaji,MUNGU wa huruma,MUNGU wa hekima,MUNGU anayetufanyia njia pasipo kuwa na njia,
kuna swali niliulizwa na mdao eti kwanini unapenda kumtaja Mungu kwenye mada zako? Mimi sikupenda kumjibu lolote,ila nilimwomba Mungu ampe uelewa yule mdau,baada ya siku mbili aliniandikia tena email nakuniambia pamoja kuwa sikumjibu amekaa na kutafakari na kupata jibu kwanini napenda kumtanguliza Mungu kwenye mada zangu.kwani sisi kama sisi hatuwezi kufanya chochote bila ya Mungu.
Ngoja nianze kuandika Mada ya leo
JIAMINI.
Ndugu mdau jiamini wewe kama wewe mwenyewe na kamwe usifikirie hatua ya kujihukumu na kujiona haufai miongoni mwajamii,kwa sababu tu umeshindwa katika jambo fulani.Amini kwamba kama umeshindwa katika jambo fulani amini kwamba,kama umeshindwa leo basi kesho ni yako ya mafanikio,usijilinganishe sana na waliokuzidi kimaisha licha ya kwamba wao ndio wakupe hasira zaidi ya kupambana,umeteleza haujaanguka
waswahili wanasema kuteleza siyo kuanguka,na kwamba tunajifunza kutokana na makosa kwa maana hyo ukiona umeshindwa kufikia malengo tambua kuwa umejifunza,na sio umekwama,ktk kushindwa zaidi kupata ujuzi na kujisafisha ukizingatia haya kesho ya furaha inakuja mbele yako.
Categories:
Unachoandika kaka ni cha muhimu sana. Maana kosa kubwa ambalo binadamu anaweza kulifanya ni kutokujiamini yeye. Kwa sababu, pengine ya kutokujielewa.
Sasa tujiulize kwa nini binadamu tunashindwa kujiamini? Maana ni kwlei wengi wetu hatujiamini. Je, tumezaliwa tuwe hatujiamini ama tunajikuta hatujiamini tunapokuwa wakubwa? Nini tatizo linaloshababisha watu kushindwa kujiamini? Malezi? Mazingira? Imani/Dini? Nini tatizo? Nauliza kupanua mjadala zaidi kwa wasomaji wenzangu.
Asante kaka kwa kuzungumzia mambo haya yanayohusu nafsi zetu wenyewe. Huwa napita hapa mara kwa mara na kusema kweli kazi zako zinastahili pongezi.
Ongeza spidi. Tuko pamoja.