Mwenyekiti mtendaji wa lpp,Reginald Mengi amesisitiza umuhimu wa watanzania kujiamini kuwa wanaweza kufanya biashara na wakafanikiwa,na kuongeza kuwa WOGA ni adui mkubwa wa maendeleo,
Mengi aliendelea kumwaga dozi za kijasiri Amali kwa kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakishindwa hata kabla ya kuanza biashara kutokana na kutokujiamini kuwa WANAWEZA,
Aliendelea kuongeza dozi pale alipogusia suala la umri
"usiseme mimi siwezi kufanya hiki kwa kuwa mimi ni mzee au kwa kuwa ni kijana,hizo ni fikra potofu umri hauwezi kukufanya ukashindwa kufanya mambo makubwa"alisema.
Akielezea kwa ufupi historia yake kidogo alisema yeye alianza biashara akiwa hana kitu laking amefika hapo alipo kutokana na kujiamini na kumtanguliza MUNGU katika mambo yote anayofanya
"ukisema huwezi mawazo yako na fikra zako zitakuelekeza kuthibitisha kuwa kweli huwez lakini ukiamini kuwa unaweza fikra zako zitakuelekeza kuthibitisha kuwa una weza na hatimaye utafanikiwa"alisema
aliongezea kuwa mtu anapaswma kuwa na wazo la biashara kabla ya kutafuta mtaji kwa kuwa kupata mtaji kabla ya kuwa na wazn la biashara anaweza kula mtaji
"ukienda mtaani ukawauliza vijana kwanini hamuanzishi biashara watakwambia hatuna mtaji,lakini kama huna wazo la biashara hata ukipata mtaji utakula,
aliwataka kushirikiana na serikali kuhakikisha vikwazo katika biashara vinaondolewa ili sekta ya biashara ikuwe.aliyasema hayo juzi usiku wakati wa uzinduzi wa shindano la wajasiri amali la kuandika michanganuo ya biashayo liitwalo
BELIEVE,BEGIN,BECOME (BBB).
SOURCE :IPP MEDIA.0
usisite kunijulisha chochote kwenye blog hii,
email gshayo@yahoo.com
bye.

Categories:

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    Hivi hizo business ideas za huku BBB zinaweza kupatatikana wapi angalau wajasiria mali tuone kama zinaweza kutufaa?

Leave a Reply