KWA WANAFUNZI WA CHUO MWAKA WA KWANZA
Unapoanza maisha ya chuo, sio tu ni mwaka wako wa kwanza katika masomo na maisha mapya ya kukua kwako, bali pia ni mwanzo wa matumizi kuongezeka. Unapo achana na wazazi na kujiunga na chuo, ni lazima uelewe umuhimu wa BUDGET. Anza kwa kujitengenezea budget na kuifuata - ni jambo muhimu sana na itakusaidia hata utakapomaliza masomo na kuanza kazi.

Unaweza kuanza chuo na ‘confidence’ kwa kuwa umesha wa ‘impress’ wazazi na jamaa kwa kufaulu vizuri, lakini, tilia maanani kuwa ‘solid habits’ za kukua kwako ni kuishi kwa urefu wa kamba yako. Tuanze leo kuzungumzia umuhim wa budget yetu, hebu tuangalie kwanza tuna kiasi gani cha kutumia kwa siku, kwa wiki au kwa mwezi.

- Anza na mkopo au ‘pocket money’ uliyonayo. Kama unapewa kwa semester au kwa mwezi, basi gawanya kwa siku 30 na utapata budget ya matumizi yako kwa siku moja.

- Pesa yeyote ya ziada unayopewa na shangazi, mjomba, kaka, nk.. ziweke benki na usizifuje. Unaweza kuziingiza kwenye budget yako au kuzihifadhi kwa ajili ya dharura. Usipende tabia ya kupiga simu home na kuomba pesa bila sababu, maana tabia hii yaweza geuka kuwa ya kudumu mpaka ukubwani. Anza kujenga ‘healthy habits’ bado mapema, ili umalizapo chuo utakuwa tayari kukabiliana na “real world.” Jitahidi kuishi kulingana na budget yako.

- Pendekeza wazazi au walezi wakutumie pesa mara moja kwa mwezi na wazideposit kwenye account yako ya benki. Kama wataamua kukutumia pesa za matumizi kwa mkupuo, mfano za miezi mitatu au sita, unapaswa uzigawe katika budget yako vizuri.

- Kama utatumiwa pesa kwa njia za mitandao ya simu, hakikisha ‘password’ yako umeitunza salama na hakuna mtu anaijua. Wizi katika pesa za mtandao hutokea kwa wingi usipokuwa makini.

- Kama una ajira ya part time huku ukiwa unasoma, ni fursa nzuri kwako kujiwekea akiba na kuacha kutumia pesa bila sababu. Mara kwa mara angalia akiba yako iliyobaki na malengo yako uliyojipangia, kama umepanga kutumia Sh.3,000 kwa siku na ukajikutua umetumia Sh.5,000 basi kesho yake jibane utumie Sh.1,000 tu.

- Kama unatakiwa kununua vitabu, bana matumizi kwa kununua 'used text books' na sio mpya. Vifaa vya dorm au hostel hununuliwa mwanzoni, usiache kuziingiza katika budget yako pia kabla hujaanza kutengeneza budget yako ya matumizi kwa siku.
Vitu muhimu vya kubudget kama unaishi nje ya chuo ni kama ifuatavyo;
- Kodi ya chumba au Hostel kwa mwezi
- Matumizi ya kila siku, sabuni, chakula, nk.
- Vocha za simu
- Photocopy na printing assignments na mahitaji ya darasani
- Kwa ajili ya matibabu unapswa ujiwekee akiba kidogo kama huna ‘Bima’ ya afya
- Usafiri wa daladala. Bodaboda na bajaji utajikuta unavuka budget yako kama hupendi usafiri wa daladala. Kama una gari lako usisahau petrol, service na insurance.
- Usisahau kubudget na pesa za usafiri wa kwenda nyumbani chuo kikishafungwa.

- Kama ni wazazi wanakulipia kila kitu, keti nao chini ili mpange budget kwa Pamoja kabla ya kwenda chuo kuanza masomo yako. Angalia kama itakubidi uwe unajipikia mwenyewe au unakula nje kwa mama lishe. Kama kuna canteen ya wanafunzi, dadisi bei ya vyakula, breakfast, lunch na dinner ili ujipange.

- Unapo discuss budget yako na wazazi, onyesha kuwa una nia ya kujipanga usikwame katika masomo yako na sio kujilimbikizia pesa. Zingatia kima cha chini cha mfanyakazi na wanawezaje kuyamudu maisha yao kwa mwezi. Hata kama wazazi wako wanao uwezo kifedha, tabia ya kuishi kwa buget ya mwanafunzi itakufunza kuishi katika mazingira halisi ya chuo. Budget yako ilingane na hali halisi ya maisha na sio ku 'over budget' au 'under budget' ukajikuta unakwama.

- Unapobakiza akiba kwenye budget yako ndipo unaweza kununua nguo, viatu au kwenda movie au gym. Hivyo vitu sio vya muhimu sana na kuviwekea budget kila mwezi kwa sababu ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi, ukisha anza kazi utavaa kila nguo unayotamani kuwa nayo.

- Vitu kama laptop ni muhimu kwa mazingira ya sasa, lakini isikuumize kichwa sana mpaka ukakosa raha kama huna laptop. Kumbuka maprofesa wote walioko chuo kikuu kwa sasa walisoma bila laptop enzi zao na walifaulu vizuri tu. Hivyo kama kila mtu amebeba laptop kwenye bega lake na wewe huna, usiji ‘stress’, nenda zako Library na utaona upana wa ‘knowledge’ unaokusubiri humo.

- Ukiweza kuishi maisha yako ya chuo kwa budget bila kuomba, kufuata mkumbo au kuishiwa, utajikuta maisha yako yamejaa furaha na muda wako mwingi uta ‘focus’ na masomo yako. Ukiishiwa pesa utakosa raha na amani moyoni itapotea, utaanza kutamani mambo yasiyo kuletea neema. Budget, budget, budget and stick to your budget! Tunakutakia siku njema!

kwa hisani ya shear illusions
Read More ...

0 comments

 
 Jiandikishe kupata taarifa mpya kuhusu nafasi za kazi > www.ZoomTanzania.com/SignUpForAlerts Hizi ni kazi 4 kati ya kazi 35 mpya zilizopostiwa  Kuweza kuona kazi zote zinazopokea maombi kwa sasa, tembelea ukurasa huu > Tanzania Jobs | Jobs in Tanzania | Tanzania Employment. Assistant Project Engineer Employer: Tanzania Portland Cement Company Limited Area: Dar es Salaam Application Deadline: July31, 2013 Position Description The Management of Tanzania Portland Cement is inviting for a suitable candidate to fill in the above vacant position. Qualification: The candidate must possess the following qualifications: Bachelor Degree in Electrical Engineering/ Power System/Automation. Good knowledge of Siemens PLC, instrumentation, basic design. Computer knowledge especially Microsoft office and Microsoft Projects. Familiar with COMPUTERIZED MAINTENANCE SYSTEM-ENTERPRISE ASSET MANAGEMENT (EAM). Minimum of ten (10) years of working experience in a cement industry or similar industries. Cement production process knowledge is an added advantage. Must be fluent in speaking and writing English and Swahili languages. Duties: Prepare scope of work for new installation(s) Prepare tender documents, feasibly study report for small installation and modification. Perform engineering and technical work related including work order, request of purchase and provide technical and analytical support, site survey for modification work and small projects. Prepare the cost estimation, analyse and compare to get the most technical- economical solution. Plan, coordinate and conduct the job efficiently. Prepare contract specification for electrical maintenance. Approve the quality of the job done by contractors. Perform any other duties that may be assigned. Click Here for full Position Description and to Apply. Branch Managers (Three Posts) Employer: DCB Commercial Bank PLC Areas: Dar es Salaam Application Deadline: July 31, 2013 Purpose of the Job From The Guardian July 23, 2013 DCB Commercial Bank PLC is a private Commercial Bank dedicated at uplifting the standard of living of .low, middle and corporate - income people in Tanzania. The bank is registered under the Companies Act. 2006 (as amended from time to time) and licensed by the Bank of Tanzania under the Banking and Financial Institutions Act, 2006. The Bank wishes to recruit the qualified personnel to fill the following vacant positions resulting from the implementation of the expansion programs taking place. The Role The Branch Manager is responsible to the Chief Manager - Banking Operations for the efficient management of. the branch in ensuring that the branch books are properly maintained, efficient and satisfactory services are rendered to customers, and ensuring that proper security arrangements are always in place to safeguard the bank's assets. Duties and Responsibilities The branch being the most important unit of the bank in delivering services to customers, the Branch Manager is responsible for maintaining the highest standard of quality customer care to enhance revenue generation. This shall strictly be done in accordance with the bank's policies and procedures and Bank of Tanzania Prudential Guidelines. He shall ensure that the branch books are properly maintained. Ensuring that all types of accounts, be current accounts, servings accounts or deposit accounts, are opened strictly in accordance to the law of banking and the country's laws and regulations in force from time to time. Ensuring that cheques and vouchers are properly drawn according to the customer's mandates held by the bank. On daily basis, shall scrutinize cheques unpaid register, accounts opened register and take the necessary corrective steps whenever mistake are detected. Ensuring the loan applications received are registered and immediately forwarded to Credit Manager for analysis and thereafter submitted to the relevant authority for approval. Ensuring that loan disbursements are carried out as per stipulations in the limit sheet. Ensuring that returns on branch operations are prepared and forwarded to Head office within the set deadlines. Click Here for full Position Description and to Apply. Lecturer (Governance & Ethics, Procurement Management)-One Post Employer: Tanzania Public Service College (TPSC) Areas: Dar Es Salaam Application Deadline: Aug 05, 2013 Position Description: The Tanzania Public Service College (TPSC) is a Government Executive Agency established in 2000 as a direct response to fill a void for a sustainable public service training institution. TPSC offers programmes that are directly linked to Government business agenda and demand driven. As the demands for the public service to offer quality services at affordable costs increase, it is imperative that the service should be staffed with competent personnel. Hence, TPSC’s core business is to develop the appropriate public service competences, which will transform the service into effective and efficient machinery that will strive to meet citizen’s needs in terms of services. TPSC’s Mission is to improve the quality, efficiency and effectiveness of the public service of Tanzania by providing comprehensive training, consultancy and applied research interventions. Currently, TPSC has campuses at Dar-Es-Salaam, Tabora, Mtwara, Singida and Tanga. The demand for TPSC’s products and services has increased over the years and there is need to staff these campuses with the right candidates, who have the knowledge, skills, attitudes and behaviors (competences) commensurate with a government owned institution. Strong belief in public service values and ethos is a paramount requisite for the right candidates. If you have the required competences for the vacancies below, you are strongly recommended to apply. It has been TPSC’s mantle to be an employer of choice. Selection process will be rigorous based on the required set of competences. We have 06 open slots in total for the following positions. Successful candidates should be prepared to be assigned to any of our five campuses. Women are strongly encouraged to apply. Duties and Responsibilities Develops and delivers short and long term courses; Conducts consultancy and research; Guides and supervises students in building up their practical and research projects; Prepares learning resources and designing training exercises for students; Develops and reviews curriculum, teaching manuals; Coaches junior teaching staff; May head on od the academic departments; and Perform any other related duties as may be assigned by his/ her supervisor. Click Here for full Position Description and to Apply. HVAC Engineers and Senior Technician Employer: Global Careers Company Areas: Dar es Salaam Application Deadline: July 27, 2013 Position Description Managing installation of air conditioning and ventilation equipment for high rise commercial building.. Please give details of projects you have been involved in: name of project, name of client, name and address of project manager, value of the project, dates of start and commissioning and be specific of your involvement. Knowledgeable of public procurement procedures applicable in Tanzania, Kenya and Uganda.. Give samples of projects you have been involved Have previously supervised several central cooling AC and ventilation projects, involving VRF and chilled water systems.. Please give details of projects you have been involved in: name of project, name of client, name and address of project manager, value of the project, dates of start and commissioning and be specific of your involvement. Good command and knowledge of AutoCAD Demonstrable contract management skills (planning, site meetings, materials procurement scheduling, preparations of claims, etc.).. Please give details of projects you have been involved in: name of project, name of client, name and address of project manager, value of the project, dates of start and commissioning and be specific of your involvement and proof that you were the project engineer on those project Please read and understand the Job Description before applying Qualified candidate should apply via the Email Link above Only short-listed candidates will be contacted Click Here for full Position Description and to Apply. ALERTS - www.ZoomTanzania.com/SignUpForAlerts VIEW ALL JOBS - Tanzania Jobs | Jobs in Tanzania | Tanzania Employment. Sisi ZoomTanzania.com tunafanya jitihada kubwa kuhakikisha tunakupa nafasi ya bure ya kutafuta mamia ya nafasi za kazi nchini Tanzania. Kama unapenda juhudi zetu za ‘site’ yetu za kukuletea kazi bora Afrika Mashariki na unataka kuungana nasi katika jitihada hizi, tafadhali tembelea Ukurasa wa Facebook wa ZoomTanzania na uwataarifu marafiki zako wote kwa “Kuupenda” Ukurasa wetu. Tembelea ukurasa wetu wa Tanzania Jobsna utafute kazi kwa vigezo mbalimbali kama mahali au aina ya kazi. kama wewe ni mwajiri na una nafasi za kazi, Zitangaze BURE kupitia www.ZoomTanzania.com ili upate Wanataaluma wa Kitanzania walioelimika na wenye ufahamu wa matumizi ya Kompyuta. Je, unatuma maombi ya kazi sehemu mbalimbali bila mafanikio au kuitwa kwenye mahojiani (interview)? Tembelea ukurasa wetu wa Tanzania Job Seekers Guidekwa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha jitihada zako za maombi ya kazi na ujiongezee nafasi ya kuitwa kwenye interview.
Read More ...

0 comments

 





Baada ya kukupa Tip#2 kwamba kila kijana anapaswa kuelewa umuhimu wa Kujithamini (Self-esteem) na Kujiamini (Confidence) na kuwa mambo haya mawili yanaweza kumjenga na kumbomoa mtu. Ukosefu wa kujithamini na kujiamini ndo mwanzo wa kuporomoka kwa mafanikio yako, tulikudokeza mbinu ya kuanzia ni kujiwekea nafsi yako katika mtazamo wa juu (positive self-talk).

Sauti inayosikikia ndani ya kichwa chako ina uwezo wa kukufanya ujithamini kwa hali ya juu katika kila hatua unayochukua kwenye mambo yako. Watu maarufu na wenye mafanikio kimataifa, mfano Oprah, Jay Z, Usain Bolt, Patrick Ngowi na wengine wengi wamekiri kuwa wanayo tabia ya ‘positive self-talk’ kwa muda mrefu sana.

Watu wenye mtazamo HASI hawaachi kulalamika hovyo, kila kitu wao hukichukulia negative. Ni wagumu kuji ‘adapt’ na hali halisi, hawana subira na hupenda kuponda kila mtu au kila kitu. Muda wao mwingi hupoteza katika kuwaza mambo yasiyoweza kuwasaidia chochote. Mara nyingi hujiangusha wenyewe kwa kuwa na mtazamo HASI na tabia ya ‘negative self-talk’. Tuangalie mambo yanayoendelea kichwani mwako, kama wewe ni katika kundi la watu wasiojiamini wala kujithamini;

- Una imani kuwa wewe hauko sawa kama mtu wa kawaida

- Unajisikia hovyo, mpweke na stress zimekujaa ndani yako

- Unajiona una mapungufu mengi mfano, mtu akikusifia “umependeza”, badala ya kusema “asante”, huku ukitabasamu, jibu lako huwa “aaah kupendeza nitapendeza mie bwana, nguo yenyewe mtumba na sura yenyewe hii kama…...”

- Unajiona kuwa thamani yako ni ndogo, mfano “mimi sifai”, “mimi mjinga – sina akili”, “kila mara nashindwa au nafeli”.

- Una mtazamo hasi juu yako binafsi na uwezo wako wa kutimiza malengo uliyojipangia, mfano –“sidhani kama nitaweza kufanikiwa hilo….” “Mimi siwezi bwana….” “Aaaah hiyo haiwezekani, haiwezi kufanya kazi”.

- Unapoteza kujiamini kwako na unaona ‘future’ ya mbele hakuna kitakachobadilika

- Una imani ndogo sana kwa vitu vilivyoko maishani mwako

- Una amini kuwa ulimwengu hauwezi kukutimizia mahitaji yako binafsi

- Una acha kujishughulisha katika kuhangaika kutimiza ndoto zako

- Unagundua kuwa huna furaha wala mafanikio kama watu wengine walio fanikiwa

- Unaona watu wengine kuwa ni bora zaidi, wenye nguvu na wana mafanikio kuliko wewe. Unawaacha wakutumie au wakusaidie mambo yako

- Unaumia chinichini, unasononeka au unasikitishwa na hao watu

- Unajiona wa hovyo, au usiye kuwa na shukrani kuwa na mawazo ya hivyo kwa hao watu

- Unajisemesha mwenyewe na kujinyamazisha. Unajiadhibu kwa kushindwa kuwa kama wengine

- Unapojitazama, unajiona kama unatumiwa na wengine ili wajinufaishe mahitaji yao

- Unajijengea kichwani mwako imani ya nguvu zaidi kuwa wewe sio mtu sawa, tena una kasoro

- Unaachana kabisa na swala zima la kujithamini na kila kukicha mambo hayo hapo juu yanajirudia upya tena na tena

Tuangalie sasa hii tabia ya kutokujithamini (negative self-talk) ina anzaje anzaje!

- Kuna baadhi ya matukio yaliyokukuta maishani mwako yanaweza kuwa chanzo cha kukuletea hali ya kutokujithamini (low self-esteem) katika maisha yako.

- Kushushwa thamani mara nyingi na kudhalilishwa – hii inaweza kutokea nyumbani, kazini, shuleni, au popote pale

- Kubeba lawama ya vitu ambavyo hujahusika wala sio kosa lako

- Kukosekana kwa kutimiziwa mahitaji yako ya msingi

- Kudhalilishwa au kuteswa, mfano mtoto kutukanwa sana au kupigwa hovyo

- Kufanyiwa udhalilishaji au mateso ya aina nyingine, mfano kubakwa au kubaguliwa

- Kuwa na "label" iliyogandishwa kwako na watu wengine, mfano mlemavu au kuambiwa una wazimu na akili zako haziko sawa

- Kupata ujumbe wa mara kwa mara kuhusu nini wazazi, walimu, n.k.. wanategemea kutoka kwako – hili linaweza kuwa tatizo zito sana kwa watu ambao mzazi wake ni mlevi

- Vitu vinavyo onyeshwa kwenye TV, Movie na matangazo ya biashara yanayo onyesha ni kitu gani kinachotarajiwa kutoka kwako na unatakiwa uwe vipi, kimaumbilie, kimavazi na kazi nzuri yenye status

Hivi ni baadhi tu ya vitu hatuwezi kuviorodhesha vyote ambavyo vina nguvu kubwa sana katika kukubomoa ‘self-esteem’ yako. Hivi vitu vinachangia katika kushusha thamani ya mtu na sio kosa lako. Vinaweza kuwa ni mambo mtu mwingine amekufanyia au jinsi mambo yalivyo katika mazingira unayoishi au uliyokulia.

Huna uwezo wa kumbadilisha mtu. Ila unao uwezo mkubwa wa kujilea, kujitunza, kujibembeleza, kujidekeza, kujipenda na kujipongeza mwenyewe na nafsi yako. Kizuri zaidi ni kuwa unayo ‘control’ KUBWA sana katika kucheza na fikra zako, mtazamo wako ndio silaha kubwa sana ya kukujenga, jinsi utakavyo ‘think’, kujisikia na kufanya kwenye maisha yako. Anza leo KUFUTA fikra zote mbaya (hasi) kichwani mwako, jaza positive things na utaanza kuona hali ya maisha yako inavyobadilika.

Tembelea ukurasa wetu kesho tukijaaliwa tutazungumzia jinsi utakavyo jikuta kwenye dimbwi la moto kama utashindwa kuachana na ‘negative thoughts’. Amini usiamini, mitizamo HASI na mambo yanayosikika kichwani mwako ni hali inayoweza kukubomoa. Tutakupa mbinu zingine zitakazokusaidia katika kujijengea tabia za kujiamini na kuachana na mawazo HASI ya kujishusha thamani. Tunakutakia siku njema!

kwa hisani y shear illusion
Read More ...

0 comments