Maisha ya biashara ili yaweze kufanikiwa vema na kuepuka kushindwa
yanahitaji ubunifu wa hali ya juu wa kipawa chako na pia uzoefu wa
huduma nzuri wa kutoka kwa watu wengine alisema Brian Adam,Hii ni kweli
kabisa kwa maana huwezi fanya kila jambo wewe,unategemea kutoka kwa
wengine,Maisha haya yote tunayoishi tunategemeana,Hivyo kama
wafanyabiashara tunahitaji msaada kutoka kwa watu wengine,Ndio maana
makampuni huwa hukodi wakala wa kuajiri wafanyakazi wapya wazuri,pia
hukodi kampuni ya kufanya usafi,kuhusika na technologia na
taarifa,kuhusika na ushauri wa kiongozi wa managementi,kutoa ushauri wa
kifedha wa kampuni nk.
Kama wewe ni mfanyabiashara unataka fanikiwa
sana inabidi uwe mwangalifu sana jinsi ya kuchagua timu kazi
utakayoshirikiana nayo kwanjia moja au nyingine ili kufikia pale
unapopataka,Hii ni timu amabyo kama mfanyabiashara unatakiwa uwe nayo:
1.Muhasibu:Muhasibu
aliyebobea na mwenye weledi juu mambo kodi ni mmoja wa watu muhimi sana
mfanyabiashara unatakiwa uwe nayo,Muhasibu atakusaidi kukuokolea fedha
kubwa ambayo ungeweza kulipa kodi pia na ni muhimu sana katika ushauri
wa uwekezaji.
2.Banki:Chagua benki ya chagua lako kwa
uangalifu,tengeneza urafiki wa karibu na manega(manager) wa benki
husika,Weka fedha zako benki mara kwa mara usijali hata ikiwa ni fedha
ndogo kiasi gani,Hii itaonyesha upo makini sana katika kuweka fedha
benki,Hiki ni chanzo cha manega(manager) wa benki kukupatia kiasi
chochote cha fedha unachokihitaji kwa ajili ya upanuzi wa biashara yako.
3.Wakala
wa bima:Bima ni chanzo cha ulizi na uwekezaji wa biashara yako,Tafuta
wakala wa bima mwenye weledi ya kazi hiyo katika hali ya urafiki
4.Wakala
wa shamba na nyumba:Biashara ya majumba imetengeza matajiri wengi sana
duniani,wengi wamekuwa waki nunua mashamba,majengo na majumba
yasiyoendelezwa kwa bei ndogo na kuyaboresha kwa gharama ndogo kisha
kuyauza kwa bei kubwa na kuwa matajiri wakubwa sana duniani,Mawakala wa
majumba na mashamba wanajua majengo gani yanauzwa na kwa bei gani na
faida yake baadae.
5.Mshauri wa sheria na mwanasheria:Mwanasheria
mwenye uwezo mkubwa na weledi mkubwa ni uwekezaji mkubwa unaweza
fanya.Tafuta mmoja kwa ushauri katika mikataba yako yote na mambo
mengine ni muhimu sana ili usije ukapata hasara kubwa sana.
6.Daktari:Hutoweza
fanya kazi siku zote kama siku ukiwa unaumwa,kuna sababu kuuumwa
tumbo,kiuono,meno,,nervous tension,vidonda vya tumbo,daktari anajua
sababu za kuumwa.Penda kumuona daktaari mara kwa mara kwa vipimo
mbalimbali ,pia jisikie vizuru na kufuata elimu daktari wako anakupati
ambayo inaenda kwenda kukusaidi kimwili na kiakili.
7.Mshauri wa
maswala ya kiroho:mshauri wa maswala ya kiroho ni muhimu sana
kukuongoza katika kujitambua,pia kukupatia ukweli juu ya mambo
mbalimbali ya kukongoza safari yako ya kiroho,kuna wakati katika maisha
unashindwa songa mbele lakini ukipata ushauri wa kiroho unaweza songa.
8.Msiri/mwaminifu
wa mambo yako binafsi:Kila mtu anahitaji walau rafiki wa kuabadilishana
ushauri juu ya mambo yako binafsi,kukupatia msaada kipindi cha dharura
na huyu ndio rafiki yako daima na hapa mara nyingi huwa mkeo au kama
mwanamke huwa mumeo au mzazi wako.
9.Mwaminifu wa mambo yako ya
biashara:Tengeneza uhusiano na wafanyabiashara wezako katika ofisi yako
au kampuni unayofanya nayo kazi,na mmoja wapo ambaye atakupatia ushauri
wa mambo mbalimbali ya biashara.
10.Wakala wa hisa:kama unataka
kuingia kwa soko la hisa unahitaji mtu amabye atakupatia ushauri wapi
ununue hisa na kipindi gani gani uuze hisa.Tengenza urafiki na mawakala
wa hisa sasa kwa kuwa hawa wana taarifa zaidi na kujua mfumo
unavyokwenda.
source: http://achieversmagazine.blogspot.com/

No comments:
Post a Comment