Wengi wanasema muda si rafiki kwa mwanadamu,wakiwa na maana kuwa jinsi
unavyowapita kasi pasipo wao kujua,mara ilikua siku,ghafla
wiki,mwezi,miezi mwaka miaka na kuna jambo amabalo analotoka akiwa mdogo
mpaka leo hatalitimia,na umri ndio unakaribia uzeeni,lakini swali
muhimu hapa kuna mtu alishwahi jiuliza kuwa yeye ana utawala muda au
muda unamtawala yeye na kuwa mtuwa au muhanga wa kupoteza muda?Siku moja
nikiwa ndani ya seminar moja mwezeshaji siku hiyo aliomba kabla ya
kuanza semina naomba tukae kwa ukimya kwa dakika tano,baada ya dakika
kupita watu wote walistaajabu walipoona wamekaa zaidi ya dakika tano za
muda waotumia Katika
mambo yao ya kawaida,mwezeshaji aliendelea kuuliza je mara ngapi
tunapata muda wa ukimya na kupangilia mambo yetu na kwenda kama
yanavyotakiwa?wengi walinisikitisha sana yeye kwa siku huwa lolote
linalotokea na yeye atajua mbele ya safari.Muda ni hazina ambayo
ikipotea hairudi tena,na pia lazima mtu anayepoteza muda siku atakuja
lipia huo muda kwa namna yeyote ile.Mara kadhaa kwa mazingira ya hapa
kwetu Afrika mimi huwa nasema
teknologia imeleta maafamakubwa sana kwa watu wasioandaliwa kwa
mabadiliko,vitu kama luninga,redio,simu,komputa ,mitandao ya
kijamii,magari,nk vyote hivi vimekuja kama bahari au mafuriko kuwazoa
watu wasiokuwa na taarifa ya tukio kabla,wanadamu wote tuna masaa 24 je
umeshawahi jiuliza katika masaa 24 umeutumia vipi kutengeneneza vitu
vipya au kuongeza dhamani katika maisha yako?mathalani mmiliki wa
kampuni chukulia Bakhersa yeye ana masaa 24 kama,kutokana na kuona masaa
ishirini na nne haya mtoshi akamua kununua masaa kutoka kwa watu
wengine kwa masaa 8 kwa kila mtu kila siku,fikiria kama kaajiri watu
1000 kwa siku yeye maisha yake ana masaa
1018 kwa siku,hapa najaribu weka maaana ya umuhimu wa muda,je wewe muda
wako wa masaa 24 unakutosha?kama sio je huo huo muda ambao haukutoshi
unautumia kwa ajili yako zaidi?au unautoa bure kuangalia
luninga,tamthilia,piga simu zisizo na masilahi,kuingia na kukaa mitandao
ya kijamii siku nzima?kama hupo katika kipengele hichi hakika dunia
inakudai deni la sababu ya kuja hapa duniani.
Kuna sababu amabazo hupelekea watu wengi kushindwa kuutawala muda vema nazo ni:
Kutokuwa na malengo;Ni ngumu sana kufanikisha jambo kama hujaweka malengo ambayo yanaeleweka mfano nini unataka,lini,wapi,kiasi gani nk
Kutokuwa na mpangilio;jambo
lisilokuwa na mpangalio unaeleweka,mtiririko mzima wa hilo jambo,dalili
hizo hupelekea jambo kuchukua muda ili kuweza kufanikiwa au
kutofanikiwa kabisa.
Uwezo wa kushindwa kusema hapana;Wote
tunapenda kusaidia wengine ili wafanikiwe kama sisi tunavyhitaji msaada
kutoka kwa wengine lakini wakati mwingine mtu utakuja jambo lipo nje ya
uwezo wake na kushindwa kushindwa kusema hapana kwa kumuonea huruma mtu
huku mtu akijua kwa kweli jambo hilo mwishoe atashindwa
kulifanikisha,pia kuharibu ratiba yako kwa ajili ya mtu mwingine mwenye
ratiba yake binafsi kwa sababu ya woga wa kusema hapana.
Kuingiliana mambo;mara
kadhaa tumekuwa katikati ya jambo fulani ghafla kitu fulani ambacho
nacho ni muhimu kikaja mfano simu ikaita,lakini simu sio kitu cha
kukutoa wewe kwenye jambo unalolifanya kupokea hiyo simu,kama ukiamua
kupokea simu hili jambo ambalo unalifanya sasa itachukuamuda wako mwingi
au hata kuanza mwanzo kwa lile jambo la awali,Maliza moja ufuate jambo
lingine.
Namna ya kufanya ili uwe mshindi katika kutumia muda vema:
Weka malengo;malengo
yakupatia ili hali yapi unaelekea,mtu mwenye malengo huwa anachukua muda
mdogo sana kufanikisha jambo fulani,tengeneza sasa malengo maishani
sasa,hakikisha sasa malengo yako yanaeleweka kwanza na wewe ,weka kipimo
kiasi gani unataka fika ili siku ya mwisho uje upime ni kiasi gani
umefanikiwa,malengo pia yanatakiwa yawe yawezekana na halisia.
Weka vipao mbele;kama
kiongozi katika ofisi,familia au kikundi unaweza kuwa una mambo mengi
yapo mbele yako ,ni salama kusema kuwa hutaweza kufanikisha mambo hayo
yote kwa pamoja,ni busara kuyapangilia mambo kwa
listi maalumu kwa kuanzia yale muhimu na kufuatia yasio na muhimu ,na
hata kama hukufanikisha yote leo yaliyobakia kesho au wakati mwingine
yawekee kipao mbele cha kwanza.
Pangilia mambo yako,ukitaka
jua mtu kama wewe unapangalia na kuokoa muda katika mambo yako tizama
ofisi yako au nyumbani kwako jinsi vitu vilivyo,mtu ambaye anadalili ya
kupoteza muda ofisini kwake kupo rafu rafu chumbani kwake vitu vipo
shaghala-bagala,mtu mwenye malengo ya kweli maishani huwa anapangalia
mambo yake ili aweze okoa muda,kama vitu vipo shaghala-bagala siku
ukitafuta kitu kidogo unaweza chukua zaidi ya siku nzima bila hata
kukipata,hivyo ni busara kupangilia mafaili,viandikio,mashine,nk katika
ofisi, nk.
Jifunze ni wakati gani wakusema hapana;Kuna wakati ni mwakafa wa kusema,majukumu kwa jamii ni jambo la kawaida sana
kama sehemu ya kurudisha kwa jamii matunda ya kipaji chako au
elimu,lakini utakuta wakati mwingine majukumu ni mengi kupita uwezo
wako,katika wakati kama huu ni
kosa kukubali wakati unajua utakuja shindwa tekeleza kwa usahihi au
kabisa,tumia hiz kanuni tatu,tambua sio kila kitu unaweza
fanya,usikubali kukubali mradi au jambo ambalo hutaweza kulifanikisha
kwa muda uliowekwa kulifanikisha,sito jifunga na mambo amabayo hahusiani na malengo na madhuni yangu binafsi ,hakika ukifuata hizi kanuni utafanikiwa sana.
Tumia vema muda ule unapokuwa unasubiri kitu au jambo fulani,usifikiri muda wa aina hii unaenda kwa faida,anza sasa kuokoa muda ukiwa unasubiria kupanda
basi,ukiwa unasafiri kwenda mkoanai,ukiwa unasubiri labda kumuona
dokta,bossi,kusubiri wezako wafike kwa
mkutano,darasani,shereheni,kanisani,meditation.Watu wenye mafanikio
hutumia vema muda ambao wanasubiria jambo fulani kutimia au tokea.
Kuna faida nyingi sana kutawala
matumizi ya muda,na hivyo kukupelekea katika mafanikio makubwaa katika
mambo unayofanya,pia ni hukupatia afya njema ya mwili na akili na jambo
lingine la muhimu sana huongeza ufanisi wa mambo unayofanya tofauti na
watu wasio tumia vema muda.
source: http://www.tanzaniaachievers.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment