Home

LISTI YA WATU WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA TANZANIA 2012

Listi hii imepangaliwa baada ya kukusanya maoni kutoka kwa watu elfu kumi,kupitia mitandao,ana kwa ana mahojiano,na pia kupitia mitandao yote ya jamii.Njia iliyotumika kuweka kipimo ni Ushawishi wa mtu juu ya sera mbambali za serikali na jamii,Nguvu ndani ya mitandao yote ya jamii,Uwezo wa kifedha na kubadilisha maisha ya raia,Ushawishi kupitia vyombo vya habari,Nguvu ya utashi wa mtu kubadili mtizamo wa jamii na kipawa cha mtu binafsi. 1.Dr Wilboad Slaa Utashi wa hali ya juu katika kushwawishi jamii,amefanya kazi nyingi sana katika kutoa maovu ya serikali,mafisadi,uwezo wa kutengeneza hoja makini ndivyo vilivyo mpatia umarufu,sababu ya yeye umarufu wake kupanda sana ni uchaguzi wa mwaka 2010 umashuhuri wake wa kutoa hoja za kugusa jamii hususa vijana wa Tanzania,pia ana nguvu kubwa sana kuliko mwanasiasa yeyote kwenye vyombo vya habari,na pia anashikilia nafasi ya nne kwa nguvu ya mitandao ya jamii baada ya january makamba na zitto kabwe.Mpaka sasa yeye ndio namba moja toka mwaka 2011 mwanzoni. 2.Benjamini mkapa Kipindi chake cha uraisi alikuwa hana uongozi wa kupitia vyombo vya habari aliwa na maneno machache,kwa kila mwisho wa mwezi alikuwa na hotuba kwa taifa na kuelezea taifa limefikia wapi,wengi inasadikiwa hawakumwelewa,ila alipoondoka baada ya hapo walioona matunda yake,hivi sasa anahusika na maswala ya kimataifa kutatua migogoro mambalimbali,pia ni anatumiwa na chama chake CCM kama mwamashishaji katika kampeni za uchaguzi za ubunge na wengi wanasema uwepo wake kwa kampeni za kikwete 2010 ulisaidia kuleta nafuu kwa kikwete na hivyo kupandisha mpaka hatua hii ya ushawishi,hivi sasa anaushawishi katika kupitisha sera mbalimbali za nchi na kimataifa,Pia ni mfanyabiashara maarufu na mwenyekiti wa taasisi ya benjamini mkapa foundation inayohusika na HIV/AIDS 3.Jakaya kikwete Ni raisi wa sasa wa tanzania,uwezo wake mkubwa wa kuwachangamkia vijana,watoto na sana sana wakima mama umempatia umarufuu sana na ushawishi kutokana na kuwa makundi haya yote baada ya kukandamizwa na mgawanyo mbaya wa madaraka,vijana na kina mama walikuwa hawana nafasi sana,Hivyo alivyotokea kikwete alionyesha kuwachangamkia vijana na kina mama na kupata uungwaji mkono sana,anafanya vema kwa mitandao ya kijamii,pia anaongoza kwa kushika namba moja kwa vyombo vya habari,Japo wengi wamekuwa wakimshtumu kuwa na uongozi wa kwenye magazeti,luninga,redio na mitandao ya kijamii.Hivi sasa anashika nafasi ya tatu kutokana na kushuka sana katika kuwa na ushawishi kwa mitandao ya kijamii na kauli zenye ushawishi wa kishindo ndani ya jamii kama mpinzani wake wilboad slaa,zitto kabwe na january makamba,Regildan mengi.Wengi wanasema ukitaka kufanikiwa Tanzania wachangamkie vijana na akina mama sasa. 4.Zitto kabwe Uwezo wake wa kupangilia hoja kwa umakini na kuisimamia,anashikilia nafasi ya pili baada ya january makamba ndani ya mitandao yote ya jamii,Pia anaushwawishi mkubwa sana kwa vyombo vya habari anashikilia nafasi ya pili,Uwezo wake wa kuwachangamkia vijana umezidi kumuongezea umarufu,hivi sasa ndio umeongezeka maradufu zaidi ya ule alikuwa nao kabla ya kuingia kwa kamati ya kupitia upya mikataba ya madini. 5.Godbless Lema Umachachari wake wa kugusa jamii sana sana vijana wa Tanzania kwa kupinga rushwa,pia ana nguvu kubwa sana ya kwenye vyombo vya habari,matukio makubwa sana yaliyo muongezea umarufu ni kuteuliwa kuwa mbunge wa arusha,maandamano ya chadema arusha,Na uwezo mkubwa wa kuwaelimisha vijana kujitambua na kujua haki zao za msingi pasipo shuruti. 6.Joseph mbilinyi Umaarufu mkubwa amezidi pata baada ya kuingia kwa siasa inasadikiwa ana uwezo mkubwa wa ushawishi kwa vijana Tanzania,wengi vijanawamekuwa wakimwangalia kama mfano kwao,na hii wataalamu wa siasa wanasema itapelekea vijana wa mziki Tanzania 2015 kuingia kwa siasa na kuweka historia itakayodumu muda mrefu,ana nguvu kubwa sana kwa mitandao ya kijamii yote,ana nguvu kubwa kwa vyombo vya habari hususa magazeti yote. 7.January makamba Ni kijana mwenye ushawishi mkubwa ndani ya mitandao ya kijamii yote,vyombo vya habari na ana utashi mkubwa wa kisiasa,ana mipangilo iliyo bora sana kuliongoza jimbo lake. 8.Samweli Sitta Ni spika wa bunge la 2005/10 alileta mabadilikomakubwa sana juu ya uendeshaji wa bunge,hivi sasa ni waziri wa africa mashariki,ana nguvu kubwa sana ya vyombo vya habari,ana ushwawishi mkubwa katika sera za Tanzania,na pia ana ushwawishi wa kiuongozi. Reginald Mengi :Mmiliki wa IPP Group of companies ana ushwawishi sana kwa jamii,sera za nchi,kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. 10.Annanilea Nkya Ni kati ya wakina mama wanaharakati hapa Tanzania,amekuwa na nguvu kubwa sana kuishwawishi jamii kujielewa haki zao,amekuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono makundi mablimbali yanaodai haki zao. 11.Freeman mbowe Ni mtu makini mwenye ulewa tosha wa utumizi wa vyombo vya habari kujibu mashambulizi ya wapinzania wake,amekuwa na sera za liberali,ana utashi mkubwa wa kiuongozi wataalamu wa uongozi wanasema ni kiongozi aliyezaliwa na sifa za uongozi,Ana ushawishi sana bungeni kauli zake ni chache lakini ndio hitimisho la hoja nyingi. 12.Mwamvita makamba Yeye ni mwenyekiti mtendaji wa mfuko wa vodacom foundation Tanzania,Pia ni afisa mkuu masoko Tanzania ana ushawishi mkubwa sana kwa vijana wa kike,pia na kiume,ana nguvu kubwa sana kwa mitandao ya kijamii na pia ana nguvu kubwa sana kwa vyombo vyote vya habari.Amekuwa mashuhuri sana kutokana na uwezo wake wa kubuni mbinu mpya ya kusaidia jamii kwa kupitia vodacom foundation. 13.Joseph kusaga mmiliki wa cloud's media group 14.Dr Rose Migiro:Naibu katibu kuu wa umoja wa mataifa anayemaliza muda wake. 15.Said salim Bakhressa:Mmiliki wa S.S.B LTD Watu wa ambao wanaweza ingia kwa listi hii muda ujayo -Efreim Kibonde -Tindu lissu -Lady jay dee -Professa shivji -Prefessa Baregu -Mohamed Dweji -Rita paulsiline -sheish sharif hamad(makamu wa kwanza wa Raisi wa zanzibar) -Dr Mohamed Bilal -Deo filikunjombe -Professa Anna tibaijuka -Edward lowasa -Salam jabir -Professa Ibrahim Lipumba -Mizengo Pinda source:http://www.tanzaniaachievers.blogspot.com/2012/04/listi-watu-wenye-ushawishi-mkubwa-sana.html

4 comments:

  1. Mwavita Makamba???????????????????????????

    ReplyDelete
  2. Anonymous kwanini hawezi kuwa miongoni mwao?

    ReplyDelete
  3. Waliopiga kura au kutoa maoni yao ni kweli yanaheshimika na nawaheshimu pia,ila wanakubalika naniii.....? kama ni wa TZ,Bro rudi kwenye UCHAGUZI,Kama kuna magumashi,kwa nini hayo maoni yao tuyaamini.......?, Nikweli lakini hatuwezi kupima ujazo wa GUNIA la mahindi kwa KAMBA tukajua ujazo wake,,,kipo kipimo chake sahihi,Haya ni yangu maoni......!

    ReplyDelete
  4. hii list inayokuja huyu kibonde sijui..

    ReplyDelete