Maisha ya mtoto yapo katika hatua ya ukuwaji kila
siku. mambo yanayomzunguka na hasa anayotendewa ndio yanayomtengeneza kuwa
jinsi alivyo kwasasa na hata baadaye. Msukumo wa nje ya mazingira yake ndio
unaotengeneza maisha yake,tabia yake,akili yake na hata uwezo wake. mtoto ni
jinsi alivyo kutokana na jinsi alivyolelewa kuwa alivyo na jinsi anavyotendewa.
Atakuwa atakavyokuwa baadaye kutokana na yale anayoyashuhudia,
anayoyaona,anayoyasikia,anayoambiwa,anayofundishwa na zaidi sana kwa
anayotendewa.
Watoto ni viumbe
vinavyokuwa kiakili, kihisia na
kisaikolojia kwa kutumia msukumo wa nje sana
kuliko wa ndani.
Ni kweli
kuwa uwezo wa mwanadamu maishani husababishwa sana na msukumo wa ndani, lakini
katika maisha ya mtoto uwezo wake hutengenezwa kutokana na msukumo wa nje kwani
anapokuwa mdogo ni kipindi cha ubongo wake kukuwa na kupewa chakula cha nje ili
kujenga uwezo wake wa ndani.
Kutokana na hayo mazingira na mambo
anayotendewa akiwa mtoto yanaweza kumtengeneza kuwa vyovyote.
Tunaishi katika jamii isiyotambua msukumo huu,
jamii isiyosikiliza sauti ya mtoto, jamii isiyo na usalama katika maisha ya
mtoto kutokana na uonevu ama unyanyasaji kwa mtoto pasipokujitambua. Na wengi
wetu hatuna uelewa kuhusu msukumo wa nje hasa uonevu unavyoweza kubadili hatima
ya maisha ya mtoto. Watoto wanayo haki ya maisha ya utoto yasio na uonevu ili
kutengeneza uwezo wa ndani ya wao kuyamudu maisha ya dunia hii ambayo kwao ni mpya.
Labda inatupasa tujue nini maana ya uonevu
kwa mtoto?
tembelea hapa kwa habari zaidi
www.treasurewithinyou.blogspot.com
http://treasurehousewithinyou.blogspot.com/2012/04/madhara-ya-uonevu-kwa-watotochild.html
No comments:
Post a Comment